Wanawake wote walioamua kupamba
sehemu zao za siri kwa kuzitoboa wanachukuliwa kuwa wamepitia ukatili wa
kijinsia ama wamekeketwa kitengo cha afya kimetanabahisha hayo.
Hata
kama mtu huyo amefikia umri wa utu uzima na ameyafanya hayo kwa ridhaa
yake,bado atahesabika kuwa alipitia ukatili wenye madhara kwa afya
yake,na inapaswa kuchukua tahadhari kubwa kuweka kumbu kumbu za watu
walio toboa sehemu zao za siri.
Lakini kujichora mwilini maarufu
kama Tattoo ama kutoboa sehemu za siri ama mwilini,kumepingwa na taasisi
ya utoboaji na uchoraji tattoo mwilini kwamba hakuna uhusiano wowote na
ukeketaji.
Na kueleza kuwa vitu hivyo viwili havichangamani
kulinganisha na kutoboa sehemu za mwili wa mwanadamu,na taasisi hiyo
wanachukulia suala la kutoboa mwili kama jambo la kaiwada na la ridhaa
anasema msemaji wa taasisi hiyo Marcus Henderson.
Zaidi ya matukio
ya ukeketaji yapatayo mia mbili yalichunguzwa na polisi wa kimataifa
miaka mitano iliyopita,na inashauriwa kama kuna mtu mmoja ana mashaka na
suala ya ukeketaji wataarifu polisi.
Watoboaji makini huwa
hawataki kuumiza wateja wao na huwa hawataki kuonesha tundu za kazi zao
na hawako tayari kumtoboa mtu aliye chini ya umri wa miaka kumi na
nane,anaeleza Mr Henderson.
Mtoboaji maarufu kutoka mjini
London ambaye ametaka ahifadhiwe jina lake, amesema kwamba wateja walio
wengi huwa wanataka kutobolewa sehemu zao za siri zisilingane na
ukeketaji.
Sihusiki na ukeketaji,nadhani utoboaji ni zaidi ya pambo mwilini ama uvumbuzi mpya wa kihisia zaidi.
Mtoboaji
huyu anadai kwamba huwa anaitekeleza kazi yake kwa ufanisi
mkubwa,kwanza huangalia picha kwa umakini mkubwa kabla hajamtoboa mtu,
na kamwe hawezi kumtoboa mtu aliye na umri wa chini ya miaka kumi na
nane.
Na wateja wake walio wengi ni wanawake na hutoboa sehemu ya siri hasa kwenye pezi la sehemu ya kati ya maungo ya mwanamke.
Ingawa
mtoboaji huyu mashuhuri mwanzoni alikuwa hakubali kutoboa sehemu za
siri za wanawake,na hii ni kutokana na maungo hao yalivyo na hatari
inayowakabili kupitia utaratibu huo.
Naye msemaji kutoka kitengo
cha afya ambaye ni mwanamke anasema kwamba,kuna changamoto kwa baadhi ya
maeneo wanawake watu wazima hutobolewa sehemu zao za siri kilazima na
maeneo mengine wasichana hulazimishwa kutobolewa.
Idadi ya wanawake waliokeketwa
nchini Uingereza inatajwa kufikia laki moja na elfu sabini,na zaidi ya
wanawake na wasichana elfu mbili na mia sita wamehudumiwa na kitabibu
tangu September na kati ya hao ,mia nne tisini na tisa walitambuliwa
January mwaka huu pekee.
Nayo serikali ya Uingereza imesema kwamba
haina mpango wa kuifanyia marekebisho sheria ya mwaka 2003 kuingiza
suala la kufanya upasuaji kwa masuala ya urembo kwenye sehemu za siri.
Kamati
teule ya wabunge katika taarifa yake imesema kwamba sheria hiyo haina
budi kubadilishwa ili kuweka wazi juu ya taratibu hizo kuwa ni kinyume
cha sheria na zaidi ni kosa la jinai kama zitafanywa kwa msichana wa
chini ya miaka kumi na nane isipokuwa kwa sababu ya afya ya akili au
kimwili.
Via>>BBC
Via>>BBC
Social Plugin