Kifo cha Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa CCM kapteni John Komba ambaye amefariki dunia akiwa hospital ya TMJ February 28 kilitanguliwa na kitu ambacho kinadhaniwa kama kilikua ni ishara ya siku yake ya mwisho.
Claudia John Komba ambaye ni mtoto wa 9 kati ya watoto 11 wa marehemu John Komba ameongea na na kuelezea baadhi ya vitu ambavyo kwao imekua kama kauli ya mwisho
kutoka kwa Baba yao ambayo aliitoa siku ya sherehe ya kuzaliwa kwake.
Claudia amesema >>>‘Taarifa
ilinifikia mida ya saa 9 akasema anajisikia vibaya ambapo wakati yupo
njiani akawa anaweweseka sana, tulipofika TMJ hospital walipofanya
vipimo walisema ameshafariki’
Swali- Kabla ya hapo kulikua na ripoti ya mzee kuugua?
Claudia John Komba:
‘Zilikuwepo baba alikua amekaa ilikua mida ya asubuhi akawa analalamika
anajisikia vibaya tukampeleka hospitali, tukagundua sukari imepanda
sana na presha imepanda sana, akatolewa akawa anaendelea vizuri’
‘Juzi tarehe 26 february ilikua siku yangu
ya kuzaliwa, akaita watoto wote akasema nataka kufanya birthday sababu
birthday nyingi huwa zinanipita nakua nipo nje, akatukusanya watoto
wote, aliongea maneno ya mwisho akatusihi watoto tupendane tusiweke
matabaka kwamba huyu mdogo huyu mkubwa alisema yeye hana mkataba na
Mungu’.
Unaweza kumsikiliza Claudia John Komba akiongea hapa chini.
Social Plugin