Picha chini hapa ni mwanamke aliyefanyiwa ukatili akiwa kafichwa sura wakati akieleza namna ilivyokuwa. |
Vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya akinamama imebainishwa
kuwa ni changamoto kwa baadhi ya wananchi wa wilayani Urambo mkoani Tabora ambapo, mwanamke mmoja amefanyiwa ukatili, wa kipigo na kuwekewa
mti katika sehemu zake za siri, kisa kikiwa ni wivu wa kimapenzi.
Akizungumza na ITV nyumbani kwa mama huyo mtendaji wa kata ya Urambo Bw. Ezekiel Marwa amesema kuwa, ukatili aliofanyiwa mama huyo ni
wa kinyama, kutokana na kupigwa sana kichwani,hali ambayo mama huyo
amepoteza kumbukumbu, pamoja na uwezo wa kufanya shughuli mbali mbali.
Aidha Bw. Ezekiel amesema kuwa, katika hali ya kushangaza ambapo
baadhi ya wanandugu walitaka kufifisha kesi hiyo kwa kumtafuta mganga wa
kienyeji, ambaye alidaiwa angetengeneza dawa ili pasiwepo na kesi,
lakini mganga huyo wa jadi, katika nyumba hiyo alimfanyia ukatili wa
ubakaji mwanafunzi wa darasa la sita.
Baadhi ya wananchi ambao siku ya tukio walikerwa na kitendo hicho
ambao walitaka kumuua mshambuliaji huyo wamesema kuwa, unyanyasaji kama
huo usifumbiwe macho na serikali bali kutoa adhabu kali kutokana na
kupoteza mwelekeo wa maisha kwa mama huyo ambaye amekuwa tegemezi.
Akizungumza kwa njia ya simu kaimu kamanda wa polisi mkoani Tabora
kamishina msaidizi Juma Bwire amebainisha tukio hilo akidai watuhumiwa
wamepelekwa mahakamani.
Via>>ITV
Social Plugin