MAAFA YA MVUA YA AJABU HUKO KAHAMA,VIFO VYAONGEZEKA SASA NI WATU 46, WAZIRI MKUU PINDA AFIKA ENEO LA TUKIO

Boga likiwa limeharibiwa na mawe ya mvua


 Barafu zilizokuwa eneo la Mwakata

Idadi ya watu waliopoteza maisha katika mafuriko ya mvua ya mawe iliyonyesha katika kata ya mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeongezeka na kufikia watu 46 huku idadi ya majeruhi waliopelekwa hospitali ikipungua baada ya kutibiwa na kuruhusiwa kuondoka.

Hayo yamebainishwa na mbunge wa jimbo la msalala Ezekiel Maige wakati akizungumza  kabla ya kumpokea waziri mkuu ambapo amesema kati ya majeruhi 91 wanne wamepoteza maisha na kufikia idadi ya vifo hadi sasa kuwa 46.

Akitoa taarifa ya serikali waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera uratibu na bunge Mh. Jenista Mhagama amesema serikali ipo tayari kuhudumia waathirika kwa misaada mbalimbali ikiwemo chakula na vifaa muhimu na kuwataka kamati ya maafa mkoa ihamishie ofisi za uratibu katika eneo la tukio ili waathirika wapate huduma kwa wakati.

Akitoa rambirambi za serikali waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda amesema serikali imekuja na timu ya waratibu watakaoratibu mahitaji kwa waathirika ili waweze kusaidiwa kwa kutumia ghala la chakula la kanda lililoko shinyanga kutoa chakula na hakuna atakayekosa chakula.

Baadhi ya waathrika wameeleza pigo walilopata kwa kuondokewa na ndugu katika familia zao pamoja na kuachwa bila  hata makazi ya kuishi achilia mbali mashamba kufagiliwa na mvua hiyo hatari ya upepo na mawe.

BOFYA MANENO HAYA KUONA PICHA ZA WAZIRI MKUU AKIWA MWAKATA KAHAMA 

AU 
BOFYA HAPA KUJUA ALICHOKISEMA RAIS KIKWETE BAADA YA KUTOKEA TUKIO HILO LA KUHUZUNISHA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post