Ni maajabu!
Mwanamke mmoja, Diana Dioniz mkazi wa Magomeni Makuti jijini Dar es
Salaam, ameangua kilio cha kuomba msaada baada ya mtoto wake aliyezaliwa
mwaka mmoja uliopita kugundulika kuwa hana ubongo wa nyuma (medulla
oblongata), hali inayosababisha shingo kulegea na macho kutoona.
Akizungumza
na gazeti hili nyumbani kwake, Diana alisema alipata ujauzito wa mtoto
huyo na kujikuta akiwa na furaha kubwa, lakini baada ya kuzaliwa na
kumpa jina la John, amejikuta akipata mateso makubwa, kwani kwa muda
wote, shingo yake inakuwa imelegea na macho yake hayaoni.
“Majirani
walinishauri nimpeleke hospitali kwa uangalizi zaidi, nilipomfikisha
Muhimbili nikaambiwa suala la mwanangu linapaswa kushughulikiwa na
daktari bingwa wa magonjwa ya watoto wa Kitengo cha Moi,” alisema
mwanamke huyo.
Aliongeza
kuwa, baada ya kupelekwa huko na kuchunguzwa ndipo ilipojulikana kuwa
na matatizo hayo, ambayo yamemfanya kuwa na wakati mgumu katika kumlea,
kwani analazimika kuwa naye karibu kwa muda wote, jambo linalomfanya
kukosa muda wa kufanya majukumu mengine.
“Hali
yangu ya kimaisha ni ngumu sana, sina msaada wowote hapa, nakaa kwa
bibi mzaa baba, mama yangu yuko kwao, kwa sababu walishaachana na baba
yangu muda mrefu na kwa sasa baba ana familia kubwa huko Mwanza.
“Ninawaomba
Watanzania wanisaidie ili mtoto aweze kukaa, pia naomba pesa kwa ajili
ya kumhudumia kupata maziwa na matumizi mengine kama kiti cha
magurudumu (wheelchair).
Aliyeguswa na habari hii awasiliane nami kwa
simu namba 0718 690219,” alisema Diana.
Na Haruni Sachawa
Social Plugin