Je ushasikia kuwa watoto ni malaika ?
Amini
usiamini mtoto wa kike alipatikana hai zaidi ya saa 14 baada ya gari
alimokuwa kutumbukia ndani ya mto uliofurika huko Utah marekani.
Kitoto
hicho chenye umri wa mwaka mmoja na nusu kilipatikana na wavuvi
kinaning'inia ndani ya gari hilo lililokuwa limepinduka ndani ya mto.
Polisi wanasema kuwa mtoto huyo alipatikana akiwa ndani ya kiti cha watoto .
Alikimbizwa hospitalini katika mji wa Salt Lake City, ambapo hali yake inasemekana kuwa imeimarika maradufu.
Mamake mtoto huyo Lynn Groesbeck mwenye umri wa miaka 25 alipatikana ameaga dunia katika kiti cha dereva.
wachunguzi
wanasema kuwa mamake mtoto huyo huenda aligonga vizuizi vya barabarani
na kutumbukia ndani ya mto Spanish Fork usiku wa kuamkia Jumamosi.
Mvuvi mmoja aliwaarifu polisi baada ya kuona kitoto kikielea ndani ya gari lililopinduka .
Askari
watatu na zimamoto wanne walioingia ndani ya maji hayo baridi
walilazimika kutibiwa hospitalini baada ya mwili wao kuganda katika
operesheni hiyo.
Via>>BBC
Social Plugin