Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAAJABU YA PETE YA KUOKOTA YALIYOMKUTA KIJANA HUYU… AISEE INAWEZEKANA HATA AKAKATWA KIDOLE

ring_sakawa
Kijana mmoja nchini Ghana huenda akakatwa kidole chake baada ya pete aliyoiokota na kuivaa kung’ang’ania kwenye kidole ambacho kimeshaanza kupuputika huku nyama zikianza kuliwa kimaajabu na kuanza kumtia hofu kijana huyo.Eric-Buabeng
Kijana huyo aliyefahamika kama Eric Buageng, alisema iliiokota pete hiyo pembeni ya barabara wakati akirudi nyumbani akitokea Kanisani na kuivaa kwenye kidole cha shahada mkono wa kulia, lakini cha kushangaza baada ya kufika nyumbani alianza kusikia maumivu kutokana na pete hiyo kumbana kidole.
Eric amesema kilichomshangaza zaidi ni wakati alipokuwa anaiokota mkono wake ulikuwa ukitetemeka na alipojaribu kuitupa hakuweza na kusikia sauti ambayo hakujua ilipotokea ikimwambia aende nyumbani, alipofika alijaribu kuitoa lakini hakuweza na kuna wakati anakisikia sauti ikumuamuru atoke nje lakini haoni mtu yeyote.
Tangu wakati huo jitihada za kujaribu kuitoa pete hiyo zimeshindikana pamoja na kwenda kwenye Hospitali mbalimbali ikiwemo ya wataalam wa Jeshi ya 37’ Military na ile ya Korle Bu Teaching bila mafanikio, katika jitohada za kuhakikisha inatoka alikutana na wachungaji mbalimbali waliomuombea lakini hakufanikiwa kuitoa.
files

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com