MABASI YAGONGANA HUKO MOROGORO WATU 7 WAFARIKI PAPO HAPO,26 MAJERUHI

 
 

Watu saba wamefariki dunia 26 wamejeruhiwa baada ya basi la Msanga Express likitokea Morogoro kwenda Mahenge kugongana na basi la kampuni ya Luwinzo lilokuwa likitoa Njombe kwenda jijini Dar es Saalam katika eneo la hifadhi ya Mikumi barabara ya Morogoro Iringa.
Wananchi walioshuhudia tukio hilo wamesema chanazo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi la Msanga Express alikua akijaribu kulipita lori ndipo bila tahadhari na kisha kutoa gari barabari wakati akikwepa ajali ya uso kwa uso ambapo aligongwa upande wa kulia ambapo watu sita walifariki papo hapo na mwingine amefariki wakati akiwanjiani kupelekwa hospitalini kupata matibabu.


Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema hadi sasa mwili mmoja tu ndio uliotambulika na miili mingine sita bado haijatambulika na imehifadhiwa katika hospitali ya St Kizito Mikumi ambapo maderava wa mabasi yote wamejeruhiwa na wanaendelea na matibabu wakiwa chini ya ulinzi ambapo kufuatia kuongezeka kwa mtukio ya ajali za mfululizo katika hifadhi ya Mikumi jeshi la polisi kwa kushirikiana na hifadhi ya Mikumi waanza kufanya opartion maalum kukagua madereva wanoendesha kwendo kasi katika hifadhi.
 
Katika hospitali ya St Kizito walikolazwa majeruhi muuguzi wa zamu Josefu Masenga amekiri kupokea majeruhi 26 na kueleza amesema hali za majeruhi wanaendelea na matibabu huku majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa wakieleza jinsi tukio lilivyotokea.



Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post