Watu
saba wamefariki dunia 26 wamejeruhiwa baada ya basi la Msanga Express
likitokea Morogoro kwenda Mahenge kugongana na basi la kampuni ya
Luwinzo lilokuwa likitoa Njombe kwenda jijini Dar es Saalam katika eneo
la hifadhi ya Mikumi barabara ya Morogoro Iringa.
Wananchi
walioshuhudia tukio hilo wamesema chanazo cha ajali hiyo ni mwendo kasi
wa dereva wa basi la Msanga Express alikua akijaribu kulipita lori
ndipo bila tahadhari na kisha kutoa gari barabari wakati akikwepa ajali
ya uso kwa uso ambapo aligongwa upande wa kulia ambapo watu sita
walifariki papo hapo na mwingine amefariki wakati akiwanjiani kupelekwa
hospitalini kupata matibabu.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema hadi sasa mwili mmoja tu
ndio uliotambulika na miili mingine sita bado haijatambulika na
imehifadhiwa katika hospitali ya St Kizito Mikumi ambapo maderava wa
mabasi yote wamejeruhiwa na wanaendelea na matibabu wakiwa chini ya
ulinzi ambapo kufuatia kuongezeka kwa mtukio ya ajali za mfululizo
katika hifadhi ya Mikumi jeshi la polisi kwa kushirikiana na hifadhi ya
Mikumi waanza kufanya opartion maalum kukagua madereva wanoendesha
kwendo kasi katika hifadhi.
Katika
hospitali ya St Kizito walikolazwa majeruhi muuguzi wa zamu Josefu
Masenga amekiri kupokea majeruhi 26 na kueleza amesema hali za majeruhi
wanaendelea na matibabu huku majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa wakieleza
jinsi tukio lilivyotokea.
Via>>ITV
Social Plugin