HII
nayo kali! Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Happy au mama
Hassan, mkazi wa Mbande jijini Dar, wiki iliyopita yalimpata mazito
kufuatia kutumbukia kwenye shimo la choo lililokuwa katikati ya chumba
anachoishi kwenye nyumba aliyopanga, Uwazi lina mkasa wote.
Tukio hilo lilitokea wakati mwanamama huyo akifanya usafi chumbani
humo na kujikuta akitumbukia kwenye shimo hilo ambalo awali lilikuwa la
choo.
MSIKIE MWENYEWE
“Nimeishi hapa kwa zaidi ya mwaka sasa lakini sikuwahi kujua kama katikati ya chumba changu kulikuwa na shimo la choo. Mbaya zaidi nimetoka kumlipa baba mwenye nyumba pesa yake ya kodi juzi tu kwa kipindi kingine.”

Happy au mama Hassan, mkazi wa Mbande jijini Dar aliyetumbukia kwenye shimo la choo.
SIKU YA TUKIO
“Siku ya tukio niliamka vizuri nikaanza kufanya usafi kama kawaida, ghafla nikajikuta natumbukia kwenye shimo. Ilibidi nipige kelele za kuomba msaada maana ilikuwa mshtuko kwangu,” alisema mwanamama huyo.
Anaendelea: “Wapangaji wenzangu waliposikia kelele walikuja kunisaidia, walitumia ngazi mbili nikaweza kutoka wakanikimbiza katika zahanati ya karibu kwa ajili ya matibabu maana nilichubuka sehemu mbalimbali za mwili.”
ALICHOSEMA BABA MWENYE NYUMBA
“Mpaka natolewa kwenye shimo baba mwenye nyumba hakuwepo, alitafutwa akaja na kunitaka nisiende polisi tuyamalizie nyumbani lakini hakunipa hata shilingi ya kusema itanisaidia matibabu,” alisema mama Hassan.

Muonekano wa nje wa chumba hicho.
HISTORIA YA NYUMA
“Baada ya ajali hiyo, kuna mtu aliniambia kuwa, awali chumba changu kilikuwa choo. Baba mwenye nyumba aliamua kuziba kwa kuweka sementi kidogo juu ili kuziba tundu lakini pia bado sehemu kubwa ya choo ilikuwa dhaifu ndiyo maana nilitumbukia.
“Aliamua kuziba choo ili kiwe chumba cha kupanga, akachimba choo sehemu nyingine.”
WOSIA WAKE
Mama Hassan aliwatahadharisha Watanzania wenzake kuwa, wanapopanga nyumba wafanye utafiti ili kubaini uhalisia wa chumba kwani visa kama vyake viko vingi.
Uwazi lilimtafuta mwenye nyumba huyo ili kumsikia anasemaje kuhusu kukifanya choo hicho kuwa chumba cha kulala lakini hakupatikana.
Na Shani Ramadhani

Social Plugin