Mwanamume mmoja amekutwa na
kuondolewa funza wapatao mia moja walio hai tena wanao kula kula puani
mwake na kuruhusiwa aende nyumbani .
Mwanamume huyo anatajwa kuwa na umri
wa miaka sitini na mitano ,na watabibu wanasema funza hao walikuwa
wamejichimbia ndani zaidi ya pua yake.
Mwanamume huyo ni mwenye
asili ya Sao Paulo, nchini Brazil,alikuwa akisumbuliwa mno na njia ya
mfumo wa hewa hasa puani ,na pua yake ilikuwa imeathiriwa na mabuu ya
inzi.
Pamoja na mambo mengine, mara kwa mara mwanaume huyo alikuwa
akilalamika kuwa kuna minyoo pia huwa inadondoka kutoka puani mwake.
Tundu za pua ni mahali ambapo vijidudu virukavyo huweza kutaga mayai yao hapo na baadaye hugeuka kuwa funza.
Na
wataalamu wa pua na koo wanasema kwamba chakula kikuu cha funza wakaao
puani ni nyama za pua na endapo mgonjwa ataachwa bila kupatiwa matibabu
,funza hao wanauwezo wa kutafuna na kuharibu kabisa mfupa wa mwanzi wa
pua,kuharibu vimishipa vya uso,pua na macho.
Na hali hiyo
ikitokea,jua kutakuwa na maambukizi kwenye ubongo na macho na kwa
kawaida husababisha ugonjwa wa uti wa mgongo na hata kifo.
Mwanaume
huyo aliamua kwenda kwenye zahanati nchini Brazil kutoa malalamiko yake
kwamba siku mbili nyuma aliona kitu kinachofanana na mnyoo ukichomoza
na hatimaye kutoka katika pua yake upande wa kushoto.
Mwanaume huyo anaishi na virusi vya ukimwi ana tatizo la ini,na kinga
yake ya mwili ilikuwa inapungua kwa kasi kubwa na alikuwa hajaanza
kutumia vidonge vya kurefusha maisha.
Miaka mitano iliyopita
alifanyiwa upasuaji wa pua yake baada ya kugundulika kuwa alikuwa na
uvimbe puani na hakuona dalili yoyote hapo kabla,ingawa kwa wiki nzima
kabla ya kuhudhuria zahanati alikuwa akitokwa na damu puani,maumivu ya
pua upande wa kushoto
Na harufu mbaya,alikuwa akishindwa kupumua sawa sawa na uvimbe ulianza kuonekana usoni na puani mwake.
Lakini baada ya kudumbukiza kijikamera kidogo puani mwake ,aligundulika Madaktari wakaanza kuwatoa funza hao kwa muongozo wa kamera iliyokuwa ikiangaza puani na kuitibu pua yake.
Iliwachukua
siku nne madaktari kuondoa uambukizo katika pua ya mwanaume huyo na
baada ya hapo madhila yake yakakoma na baada ya uangalizi wa mwisho kwa
kutumia kamera ile ile imethibitika kwamba tatizo lake lime kwisha.
via>>BBC
Social Plugin