Ndege moja ya shirika la ndege la British Airways imelazimika kutua kufuatia harufu mbaya iliyokuwa ikitokea kwenye choo cha ndege hiyo.
Ndege hiyo ya BA ilikuwa ikielekea Heathrow Uingereza kutoka Dubai safari ambayo kwa kawaida huchukua saa saba.
Abiria
mmoja aliyekuwa ndani ya ndege hiyo bwana Abhishek Sachdev, aliandika
kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter kuwa:
''Amini usiamini ndege yetu ya British Airways imelazimika kurejea dubai baada ya wahudumu kugundua kuwa harufu mbay inatokea kwenye choo ya ndege hiyo.
''Amini usiamini ndege yetu ya British Airways imelazimika kurejea dubai baada ya wahudumu kugundua kuwa harufu mbay inatokea kwenye choo ya ndege hiyo.
''Yamkini
rubani wa ndege hiyo aliwaita msimamizi wa wahudumu wa ndege hiyo ndipo
tukang'amua kuwa kulikuwa na tashwishi katika safari yetu''Sachdev
alinukuliwa na gazeti moja.
''mara tukaelezwa na rubani kuwa harufu mbaya ndani ya ndege hiyo inatokea kwenye choo kichafu na kuwa ilikuwa ni ya kinyesi''
''Kufikia wakati huo ilikuwa ni takriban nusu saa tangu tupae angani kwa hivyo tukalazimika kurejea Dubai''
''Ajabu ni kuwa hakukuwa na ndege mbadala ya kuturejesha London kwa hivyo ikatubidi kusubiri kwa zaidi ya saa 15 .
Hata hivyo walitupeleka hotelini tukapumzika usiku kucha''.
Mwakilishi
wa ndege hiyo Greg James, Sarah, aliiambia Radio 1 kuwa hilo halikuwa
suala la kufanyiwa utani kwani ukiwa ndani ya ndege ni tishio kubwa kwa
afya ya rubani na abiria kwa jumla.
''Ndani ya ndege huwa
kuna utupu wa hewa kwa hivyo asilimia 50 ya hewa inayotumika ni ile ile
kwa hivyo harufu mbaya ingeathiri vibaya afya ya abiria ndiyo sababu
ndege hiyo haikuwa na budi ila kurejea iliisafishwe''.
Hata hivyo shirika hilo la ndege liliomba msamaha kwa usumbufu wowote kwa abiria wake walioathirika siku hiyo.
via>>BBC
via>>BBC
Social Plugin