Mama mmoja amedai kuwa yeye na
marafiki zake wawili wamezuiliwa kuingia katika kilabu moja ya burudani
kwa sababu zinazodaiwa kuwa ni wanene sana na wenye sura mbaya
Stacey
Owen 33, alikuwa ametoka na marafiki zake wawili kwa ajili ya kupata
burudani wakati wa usiku siku ya Jumamosi alipokataliwa kuingia katika
baa moja jijini Manchester kwa sababu ya unene wake.
Stacey amesema wao walizuiwa huku watu wengine wakiingia katika baa hiyo maarufu mjini humo.
Mama huyo sasa anataka kuombwa radhi na wamiliki wa Baa hiyo lakini mpaka sasa amedai hajapata ujumbe wowote kutoka kwao.
Anasema sio kwamba anajiona kwamba yeye ni mrembo sana lakini kilichomshangaza ni uwepo wa ubaguzi huo miongoni mwa wateja.
Via>>BBC
Social Plugin