Makubwa Haya!! WAKATAZWA KUINGIA KLABU YA BURUDANI ETI KISA WANENE SANA NA WANA SURA MBAYAAA!

klabu ya burudani nchini Uingereza
Mama mmoja amedai kuwa yeye na marafiki zake wawili wamezuiliwa kuingia katika kilabu moja ya burudani kwa sababu zinazodaiwa kuwa ni wanene sana na wenye sura mbaya

Stacey Owen 33, alikuwa ametoka na marafiki zake wawili kwa ajili ya kupata burudani wakati wa usiku siku ya Jumamosi alipokataliwa kuingia katika baa moja jijini Manchester kwa sababu ya unene wake.

Stacey amesema wao walizuiwa huku watu wengine wakiingia katika baa hiyo maarufu mjini humo.

Mama huyo sasa anataka kuombwa radhi na wamiliki wa Baa hiyo lakini mpaka sasa amedai hajapata ujumbe wowote kutoka kwao.

Anasema sio kwamba anajiona kwamba yeye ni mrembo sana lakini kilichomshangaza ni uwepo wa ubaguzi huo miongoni mwa wateja.
 Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم