Picha ya kushtusha imeachiliwa kwa
ulimwengu hivi karibuni picha inayomuonesha mtoto mdogo mwenye umri wa
miaka mitano aliye kondeana ,aliyetelekezwa katika sehemu ya chini ya
nyumba yao ,aliyefungiwa na kuachwa afe njaa na familia yake.
Tammi
Bleimeyer,mwenye umri wa miaka 33,na mumewe Bradley,mwenye miaka 24,
wameshtakiwa kwa kosa la kuhatarisha uhai wa mtoto wao baada ya kumkuta
mtoto huyo akiwa katika hali dhoofu katika majira ya baridi ,kitongoji
cha Harris, huko Texas.
Askari aliye fanikisha kupatikana kwa
mtoto huyo Mark Herman,amesema kwamba amefanya kazi ya polisi katika
kipindi cha miaka thelathini lakini hajawahi kushuhudia tukio lanamna
hii.
Askari huyo anasema wamemkuta mtoto huyo katika hali mbaya
ana njaa kali,amekondeana,amevilia damu mwilini kama aliyekuwa akipigwa
ama kupitia mateso makali na ngozi yake ilionekana kama imeachana na
mifupa ,ilikuwa ni hali ya kutisha sana kumwona mtoto katika hali hiyo.
Bradley
alikuwa akibishana na mtoto huyo wa kambo mwenye umri wa miaka kumi na
sita aliyekuwa akiwataka wazazi wa mtoto huyo kuacha kumfungia mtoto
wako katika chumba cha chini ya ardhini nyumbani mwao .
Na polisi
walipofika nyumbani hapo waligundua chumba kidogoo,chini ya nyumba hiyo
kikiwa kimefungwa na godoro tu ndani yake na mtoto aliyeketi juu ya
godoro ,ingawa mama wa kambo wa mtoto huyo alimtorosha baada ya kujua
kwamba polisi wanamfuatilia, na kumkuta katika chumba cha hoteli na
kumfuatilia hatimaye kumchukua mtoto huyo na kumpeleka hospitalini kwa
matibabu.
Ingawa mpaka mtoto huyo anafikishwa hospitalini, sababu
za kufungiwa kwa mtoto huyo hazikufahamika mara moja ,na wazazi wa mtoto
huyo wamekataa kuzungumzia tukio hilo .
Baba wa mtoto huyo
anashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo, na mtoto wake bado
amesalia hospitalini kwa matibabu zaidi katika hospitali ya watoto
iliyoko mjini Texas
Via>>BBC
Social Plugin