Stori ya mashabiki kujiua eti kisa timu
yake imefungwa ama ina matokeo mabaya kwenye ligi sio ngeni kuzisikia..
Wapo ambao wanashindana wanaweka nyumba au hela, timu yake ikishindwa
ishu inakuwa story tofauti.
Taarifa kutoka Kaunti ya Kilifi pwani ya
Kenya mtu moja amejitoa uhai kwa kujitosa ndani ya bahari ya hindi kutoka
kwa Daraja la Kilifi baada ya kukasirishwa na matokeo ya Robo fainali
kombe la FA baina ya mahasimu wakubwa Uingereza Arsenal na Man United iliyochezwa Jumanne usiku.
Mtu ambaye alizungumza na jamaa ambaye amejiua amesema kabla ya mechi shabiki huyo alikuwa akijigamba jinsi Man U watakavyowaadhibu Arsenal, lakini hali ikawa tofauti.
Ishu iko mikononi mwaPolisi ambao wanendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
Social Plugin