Shuti safi la Mbwana Samatta limeiwezesha Taifa Stars kuokoka na aibu baada ya kupata sare ya mabao 1-1 dhidi ya Malawi.
Katika
mechi hiyo ya kirafiki iliyopigwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza, Malawi walipata bao lao mapema katika dakika ya 3 kupitia
kwa Esau Kanyenda.
Kanyenda
alifunga bao hilo baada ya kipa Mwadini Ally kushindwa kuupangua mpira
vizuri. Halafu mabeki nao wakashindwa kuondosha hatari.
Stars
ilishindwa kucheza vizuri hadi kipindi cha pili Mrisho Ngassa na Salum
Abubakari ‘Sure Boy’ wakichukua nafasi za Harun Chanongo na Amri Kiemba.
Samatta alifunga bao hilo baada ya pasi nzuri ya Ngassa ambaye alimpiga chenga beki mmoja na kupiga krosi safi ya chinichini.
Mechi hiyo ilikuwa katika kalenda ya mechi ya kirafiki ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Social Plugin