Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando (kushoto) na Mkurugenzi wa Operesheni ya Uchaguzi wa Chadema, Benson Kigaira |
MABERE
Marando- Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Madendeleo
(Chadema), amefichua mawasiliano ya siri yanayofanywa na vyombo vya dola
dhidi ya chama, na mkakati wa kumdhuru Katibu Mkuu, Dk. Willibroad
Slaa. Anaandika Sarafina Lidwin.
Amesema kuwa Idara ya Usalama wa Taifa na Makamu Mwenyekiti wa CCM
Taifa, Philip Mangula, wamekuwa wakimtumia Khalid Kagenzi-mlinzi binafsi
wa Dk. Slaa ili kurekodi na kuvujisha taarifa za vikao vya siri vya
Chadema.
“Kama chama tumelalamikia sana serikali ya CCM kwa matumizi mabaya ya
vyombo vya dola dhidi yetu. Sasa tumebaini wanatumia vijana wetu kunasa
taarifa zetu.
“Kagenzi kwa miaka miwili tumebaini amekuwa akitumika kupeleka taarifa
za Chadema kwa usalama wa taifa. Amekiri hilo kwa maandishi na kutaja
namba za watu wa usalama anaowasiliana nao,” amesema.
Marado alimtuhumu Mangula kuwa imebainika anawasiliana na Kagenzi ikiwa
ni pamoja na kumtumia fedha mara mbili, Julai 24 na Desemba 4 mwaka
jana, kupitia simu yake ya Vodacom (anaitaja).
Kwa mujibu wa Marandu, mlinzi huyo alipobanwa zaidi alieleza mkakati
uliokuwa ukipangwa na watu hao wa kumwekea Dk. Slaa sumu kwenye chakula
au kinywaji.
Amesema
kuwa wamebaini nyendo hizo hivi karibuni baada ya mlinzi huyo kuonekana
akipanda katika gari ya afisa usalama wa mkoa wa Kinondoni lenye namba
za usajili T213 ARS, akiwa nalo afisa msaidizi.
Marando
amefafanua kuwa watamfikisha Kagenzi polisi ili achunguzwe na hatua
zaidi zichukulie, lakini akakataa kuweka hadharani namba za simu na
majina ya maafisa usalama aliodai wako zaidi ya 22.
Amesema kuwa pia wamenasa taarifa za maofisa hao za kumtumia Kagenzi
muda wa maongezi zaidi ya shilinigi milioni saba kwa nyakati tofauti.
via>> mwanahalisi Online
Social Plugin