Masheikh zaidi ya 50 kutoka Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, leo
wamemkabidhi kiasi cha shilingi 700,000/- za kuongezea kuchukua fomu ya
kuwania urais 2015.
Mashekhe hao wakiongozwa na Yusuf Surulu na
Alli Mtumwa wamemkabidhi fedha hizo nyumbani kwake mjini Dodoma na
kushuhudiwa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof Juma Kapuya.
wamesema kuwa wameona mtu pekee anayefaa kushika wadhifa huo ni yeye
hivyo wanamsihi atangaze nia na achukue fomu ya kugombea na wapo nyuma
yake katika dua.
Lowassa amewaambia viongozi hao wa dini kuwa makundi mbalimbali ya jamii yamekuwa yakimuomba kugombea Urais lakini wao wamemfanya ashawishike sasa kufanya hivyo wakati ukifika.
via>>EATV
Lowassa amewaambia viongozi hao wa dini kuwa makundi mbalimbali ya jamii yamekuwa yakimuomba kugombea Urais lakini wao wamemfanya ashawishike sasa kufanya hivyo wakati ukifika.
via>>EATV
Social Plugin