Maria Ionita akiwa na mumewe, Florin Ionita hospitalini.
MWANAUME aitwaye Florin Ionita, 53, ameng'atwa sehemu yake nyeti na
rafiki wa mkewe wakati akijaribu kumlazimisha afanye naye mapenzi.
Wauguzi waliokuwa wakimpatia huduma Florin Ionita.
Florin Ionita na mkewe Maria Ionita, 49, walikuwa katika karamu huko Chisinau nchini Moldova wakiwa na rafiki wa mkewe.
Baada ya karamu hiyo, Maria aliamua kuwapeleka baadhi ya marafiki zake
nyumbani kwao huku nyuma akimuacha mumewe akiwa na rafiki yake mwenye
umri wa miaka 24.
Florin Ionita akiendelea kupatiwa huduma baada ya kung'atwa nyeti zake.
Cha kushangaza baada ya dakika 30, Maria alirudi eneo la karamu kumfuata
mumewe na kukuta akilia kwa maumivu na kumwambia: "Niitie gari la
kubeba wagonjwa, sehemu yangu nyeti itadondoka"
Kufuatia tukio hilo, Maria alitaka kujua kilichotokea ndipo rafiki yake
akamweleza kuwa mumewe alimlazimisha afanye naye mapenzi na kuvua
suruali ndipo akaamua kujihami kwa kumng'ata sehemu zake nyeti.
Maria aliamua kumsamehe mumewe kwa kusema: "Nimemsamehe maana alikuwa
akijaribu kufanya kitendo ambacho wanaume wengi hutaka kukifanya, ila
nilipowapigia watu wa gari la kubeba wagonjwa sikufanya haraka, na
niliwaambia wasifanye haraka sana kufika eneo hilo"
Mwanamke huyo mbali na kuwaambia wasifanye haraka watu wa gari la kubeba
wagonjwa, pia aliwatajia eneo ambalo si husika ili kumpa fundisho
mumewe huyu mchepukaji.
Social Plugin