Siku chache tu baada ya kutokea gharika ya mvua ya upepo na
mawe yenye uzito unaodaiwa kuwa ni kilo 20 na kuua watu wengi ,mifugo na kuharibu
mazao katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga,Msanii
maarufu wa nyimbo za asili nchini Tanzania,Bhudagala Mwanamalonja akiwashilikisha wasanii wa mkoani Simiyu, ametoa wimbo wa kuwapa pole wakazi wa kijiji cha Mwakata kutokana na maafa hayo.
Wimbo huu maalum umefanyiwa production na studio za Bujiku Faster Recordz zilizoko wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Wimbo huu maalum umefanyiwa production na studio za Bujiku Faster Recordz zilizoko wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Akizungumza na Malunde1
blog leo baada ya kuachia wimbo huo Bhudagala amesema Video ya wimbo huo unaoitwa Maafa Mwakata itatoka ndani ya siku 5 kuanzia leo
Jumapili Machi 15,2015.
Sikiliza
na Download wimbo huo hapa chini(chagua njia moja kati ya hizo hapo 2)
Social Plugin