Licha ya Serikali, jamii na jumuiya ya kimataifa kukemea ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), bado kuna wanaoendelea kung’ang’ania mila potofu za kuamini kwamba bila ya ushirikina unaohusishwa na matumizi ya viungo vya albino, hawawezi kufanikiwa kimaisha, iwe katika kisiasa au kibiashara.
Hayo
yanathibitishwa na kuendelea kuripotiwa kwa matukio ya ukatili dhidi ya
albino, ambapo usiku wa kuamkia jana, watu wasiojulikana walimshambulia
na kumkata kiganja mtoto mwenye umri wa miaka sita, Baraka Cosmas na
kisha kutokomea nacho kusikojulikana.
Tukio
hilo lililotokea katika kijiji cha Kipeta Bonde la Ziwa Rukwa wilayani
Sumbawanga, ambako mtoto huyo anaishi na wazazi wake, Cosmas Yoram (32)
na Prisca Shaaban.
Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda.
Alisema
tukio hilo ni la saa 8 usiku wa kuamkia Jumapili wakati mtoto huyo
akiwa amelala na mama yake. Baba wa mtoto huyo hakuwepo wakati huo.
Akielezea
zaidi, Kamanda Mwaruanda alisema usiku huo kikundi cha watu
wasiojulikana walivamia nyumba alimolala Baraka na mama yake mzazi,
Prisca wakiwa na silaha za jadi, ikiwemo mapanga na fimbo na kuanza
kumshambulia kwa kumcharaza viboko Prisca baada ya kukataa kuwapatia
mtoto huyo, mwenye ulemavu wa ngozi.
“Baada
ya kuingia ndani ya nyumba hiyo walimwamuru mama mzazi wa mtoto Baraka
kuwakabidhi mtoto huyo, lakini alikaidi ndipo walipoanza kumshambulia
kwa kumpiga kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na kumjeruhi
vibaya …
“Waliingia ndani baada ya kuvunja mlango wa nyumba hiyo, ndipo katika patashika hiyo wavamizi hao walimkata mtoto Baraka kiganja cha mkono wake wa kulia na kuondoka nacho kusikojuliakana,” alibainisha.
“Waliingia ndani baada ya kuvunja mlango wa nyumba hiyo, ndipo katika patashika hiyo wavamizi hao walimkata mtoto Baraka kiganja cha mkono wake wa kulia na kuondoka nacho kusikojuliakana,” alibainisha.
Aliongeza
kuwa wakati hayo yakitokea, baba mzazi wa mtoto huyo inadaiwa alikuwa
amelala katika nyumba ya mkewe mdogo kijijini humo.
Kwa
mujibu wa Mwaruanda, mtoto huyo amelazwa katika katika Kituo cha Afya
cha Kamsamba wilayani Momba mkoani Mbeya kwa matibabu akiwa pamoja na
mama yake mzazi.
“Watu
watatu ambao majina yao yamehifadhiwa, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi
mkoani hapa kwa mahojiano na uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo
unaendelea ili kuwasaka wahusika na kiungo hicho cha kiganja cha mkono
wa mtoto Baraka,” alisisitiza Kamanda.
Via~Mpekuzihuru
Watoto wenye ulemavu wa ngozi (Albino)
Matukio ya ukatili dhidi ya albino yanaendelea kuwa tishio nchini
Tanzania baada ya mtoto wa miaka sita kukatwa kiganja cha mkono
Shambulio hilop jipya limetokea mkoani Rukwa kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Mtoto huyo kiume Baraka Cosmas alikuwa amelala na mama yake mzazi wakati wahalifu hao walipovamia nyumba yao.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa Jackob Mwaruanda amesema kwa sasa mtoto
huyo anapata matibabu hospitali na hali yake inaendelea vizuri.
Polisi inaendelea na uchunguzi kubaini wahusika.
Shambulio hilo linajitokeza wiki moja tu baada ya watuhumiwa wanne
kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa mauaji ya albino, Na muda mfupi baada ya
Rais Tanzania Jakaya Kikwete kukemea mauaji ya albino, ambao viungo vyao
hutumika katika shughuli za kishirikina kwa imani potofu kuwa
zinasaidia kuleta utajiri na madaraka.
- See more at: http://jaladakuu.blogspot.com/2015/03/mtoto-mwingine-albino-akatwa-kiganja.html#sthash.MTRouF6K.jGUzg0eU.dpuf