Mkazi wa Nyakato
wilayani Kahama mkoani Shinyanga Elias Charles(30) amekutwa amejinyonga
nyuma ya mlango nyumbani kwake kwa kile kinachodaiwa kukwepa deni
alilokuwa akidaiwa.
Kamanda wa Polisi mkoa
wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema tikio hilo limetokea juzi asubuhi,
na kwamba Charles amejinyonga kwa kile kinachodaiwa kukwepa deni la
shilingi laki 1 na nusu alilokuwa akidaiwa na ndugu zake.
Akifafanua tukio hilo
Kamugisha amesema mke wa marehemu Regina William(30) alitoka kwenda
kuoga na aliporudi akamkuta mumewe amejinyonga nyuma ya mlango wa nyumba
yao kwa kutumia kamba ya Manila.
Kamugisha amesema
Uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na mke wa
marehemu, umedai Elias amejinyonga kutokana na deni alilokuwa akidaiwa
na ndugu zake tangu mwaka jana na si ugomvi na mkewe kama inavyodhaniwa.
Mwili wa marehemu
umehifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya
Kahama, huku jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa kina juu ya
tukio hilo.
Social Plugin