Watu wakishuhudia gari lililogongwa.
Ajali hiyo ikiwa imesababisha foleni kubwa.
AJALI mbaya imetokea leo mchana kati ya Toyota Mark
II na Toyota Prado eneo la Msimbazi Centre jijini Dar kufuatia gari aina
ya Prado lililokuwa likitokea Magomeni kuelekea Boma kugonga gari dogo
lililokuwa likitokea Ilala Boma.
Ilikuwa hivi; Gari aina ya Prado ilikuwa ikitokea maeneo ya Kigogo
Mbuyuni (Round about) kuelekea Msimbazi Centre, lilipofika kwenye bonde
la Msimbazi, kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha, dereva
aliyekuwa mwendo kasi alishindwa kuona mbele hivyo kujikuta akivuka tuta
lililo katikati ya barabara na kwenda upande wa pili ambako lilikutana
na gari aina ya Toyota Mark II na kuligonga sehemu ya mbele.
Hata hivyo, hakuna aliyeumia katika ajali hiyo na mwandishi wetu
alipofanya jitihada za kuwasaka madereva wa magari hayo hawakuweza
kupatikana.
CHANZO-GPL
CHANZO-GPL
Social Plugin