MVUA YA AJABU ILIYOUA WATU 46 SHINYANGA INAITWA "TONADO", NI MARA YA KWANZA KUTOKEA TANZANIA


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Agnes Kijazi amesema mvua iliyonyesha Shinyanga na kusababisha maafa kwa jina la kitaalamu inajulikana kama ‘Tonado’, ni mara ya kwanza kutokea hapa nchini.


Kijazi alisema katika ofisi za mamlaka hiyo wakati wa ziara ya Kamati ya Wabunge ya Miundombinu, jijini Dar es Salaam.

Alisema utabiri waliokuwa wameutoa wa saa 24 ulionesha kutakuwa na mawingu mazito katika eneo hilo, lakini hawakutarajia Tonado kunyesha kwa kuwa sio mfumo wa
kawaida kwa hapa nchini.

Kijazi alisema kutokana na mabadiliko ya tabianchi kumekuwa kukiongezeka matukio ya hali mbaya ya hewa hata ambayo awali yalikuwa hayatokei.

Alisema Tonado, kitaalamu ni mawingu mazito yenye unyevunyevu ,yanapozidi uzito yanaanguka mabarafu, hivyo kutokana na mabadiliko hayo upepo mkali unaozunguka sio hali ya kawaida katika maeneo ya tropiki.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post