Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWALIMU ABURUZWA MAHAKAMANI KWA KUBAKA MWANAFUNZI WAKE USIKU WA MANANE!



Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Joseph Konyo.

Jeshi la polisi wilayani Chato mkoa wa Geita, limemfikisha kizimbani mwalimu wa shule ya sekondari Makurugusi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha pili.
Mwalimu huyo, Iddy Gerald (21), anatuhumiwa kufanya ubakaji huo Machi 23 mwaka huu saa 7:45 usiku ndani ya chumba chake kilichopo katika kijiji cha Makurugusi.

Mbele ya mahakama ya wilaya ya Chato, mwendesha mashitaka ambaye pia ni mkaguzi wa polisi wilayani humo, Semeni Nzigo, ameieleza mahakama hiyo mshitakiwa amefanya ubakaji huo wakati akifahamu ni kosa kisheria kufanya mapenzi na mwanafunzi.

Amedai mwalimu Idd alikamatwa usiku wa manane akifanya mapenzi na mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) bila ridhaa yake huku akiwa na umri wa miaka 16 kinyume cha sheria.

Hata hivyo, mshitakiwa huyo alikana tuhuma hizo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Jovith Katto, lakini amerudishwa mahabusu hadi Aprili 9 mwaka huu baada ya kukosa wadhamini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com