Jeshi
la Polisi limelazimika kuwatawanya wananchi kijiji cha Mkambarani
Mikese wilayani Morogoro baada ya kufunga barabara ya Morogoro Dar es
Salaam kufuatia tukio la ajali ya gari ndogo aina ya Toyota mark ii
kugonga wapanda pikipiki na kusababisha kifo cha mama mmoja mwalimu wa
shule ya msingi Mkambarani.
Vurugu hizo zimedumu kwa muda ambapo wananchi walipanga mawe
barabarani na kuzuia magari yanayotumia barabara hiyo wakilalamikia
kuchoshwa na matukio ya ajali za mara kwa mara katika eneo hilo
wakiitaka serikali kuweka matuta.
Kufuatia vurugu hizo za wananchi, serikali ya kijiji na mkuu wa
polisi wilaya Zuberi Chembela na wamelazimika kutuliza wananchi hao
waliokuwa wakizungumza kwa jazba na kuwaahidi jeshi la polisi litaweka
ulinzi katika eneo hilo kuzuia matukio ya ajali.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema chanzo cha
tukio ni gari ndogo kugonga wapanda pikipiki Godwini Mbena na alikua
amempakiza mkewe Judith Mbega mwalimu wa shule ya msingi Mkambarani
ambaye alifariki dunia na mumewe amejeruhiwa na kulazwa katika hospitali
ya mkoa wa Morogoro.
Amesema jeshi la polisi litawachukulia hatua wananchi waliohusika kufanya vurugu za kufunga barabara.
Amesema jeshi la polisi litawachukulia hatua wananchi waliohusika kufanya vurugu za kufunga barabara.
via>>>ITV