Mwanafunzi
wa shule mjini Cairo amepigwa hadi kufa siku ya Jumapili na mwalimu
wake ambaye kwa sasa amefukuzwa, wizara ya elimu ya Misri imesema
imeanza uchunguzi.
Kijana huyo, 12, alifariki Jumapili “baada ya kupigwa na mwalimu siku iliyopita”, ilisema taarifa ya wizara.
Taarifa hiyo ilisema mwalimu huyo amefukuzwa na “uchunguzi wa kina” umeanza kufuatia mazingira ya kifo cha mtoto.
Mtoto
huyo alikuwa na majeraha ya kichwani na alipatwa na matatizo ya ubongo,
mchunguzi wa idara ya vifo Hisham Abdel Hamid aliiambia AFP.
Adhabu
ni jambo la kawaida katika shule za Misri, ambapo uzembe umetajwa
kutokana na vifo vya watoto wawili mwishoni mwa 2014 kutokana na
matumizi mabaya ya vifaa.
Social Plugin