Mwanafunzi
mmoja ambaye umri wake ni miaka 17 Marekani amelazwa baada ya kupata
ugonjwa wa kupooza baada ya kula chocolate aliyonunuliwa na marafiki
zake ambao wanasoma darasa moja katika shule ya Benjamin Banneker High
School huko Brooklyn.
Mwanafunzi huyo Danieel Buchanan aliletewa chocolate na
wanafunzi wenzake ambavyo walikula wote, muda mfupi baadae hali ilikuwa
mbaya akapelekwa Hospitali ambapo muda mfupi baadae mtoto huyo
aliruhusiwa kuondoka na wazazi wake.
Muda mfupi baadaye hali ya Buchanan
ilibadilika tena, akashindwa kuongea, kutembea, kula na miguu yake
kupooza..
Mama yake akaamua siku ya pili yake kumpeleka Hospitali ya
Mount Sinai ambapo baada ya kufanyiwa vipimo ilionekana kuwa kwenye
chocolate aliyokula kulikuwa na bangi, rafiki ambaye alimpa Buchanan chocolate hiyo alisimamishwa shule anayosoma huku Polisi wakiendelea na upelelezi.
Social Plugin