Muonekano wa mwanamke huyo sehemu aliyopigwa jiwe |
Hekaheka
ya leo inatokea Ngokolo mjini Shinyanga, inahusu mwanamke aliyepigwa na jiwe kichwani na
kujeruhiwa kwenye sikio kwa kutuhumiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mume
wa mtu.
Inaelezwa kuwa mume na mke walishirikiana kumpiga mwanamke huyo hali ambayo imezua gumzo mtaani kwani ni jambo la kushangaza kuona mume anayetuhumiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine kushirikiana na mke wake kutembeza kichapo.

Mwanamke huyo aliyepigwa amesema kuwa alitoka
kumsindikiza mgeni wake wakati anarudi akapata lift ya pikipiki lakini
ghafla alishangaa kupigwa jiwe na watu anaowafahamu ambao ni mtu na mke
wake wakazi wa Ngokolo.
Mwanamke huyo amesema baada ya kupigwa
walisimama ili kuwauliza kwa nini wampige jiwe lakini waliwakimbia,
wakaenda mpaka nyumbani kwa watu hao, lakini hakuweza kuongea nao kwa
kuwa walijifungia mlango ndani.
Mwanamke anayetuhumiwa kumpiga jiwe
amesema sio kweli kwamba alimpiga jiwe mwanamke huyo na wala hakuwepo
kwenye ugomvi huo kwa kuwa yeye alikuwa amelala hivyo hajui chochote.
Mmoja ya mashuhuda wa tukio hilo
wanasema ni kweli waliomuona mwanaume na mke wake waliorusha mawe na
baada ya kurusha mawe hayo walikimbia kwenda kujifungia ndani ya nyumba
yao.
SIKILIZA HAPA CHINI
Social Plugin