Watu wasiojulikana wamemuua kwa kumchinja mkazi wa kitongoji cha Kanoge kata ya Usisya wilayani Urambo mkoani Tabora.
Mwenyekiti wa serikali ya kujiji cha Mabunduru
pamoja na ndugu marehemu wameelezea kusikitishwa kwao na kitendo hicho ,
kwani baada ya kumuua katika nyumba yake,watu hao hawakuchukua
chochote.
Diwani wa kata ya Usisya Mheshimiwa JAFARI KANKILA amesema tukio
hilo ni la pili la wanawake kuuawa kwa kuchinjwa na ameahidi kutoa
zawadi ya shilingi laki mbili kwa atakayetoa taarifa za kukamatwa kwa
wahusika wa mauaji hayo.
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Tabora Kamishina
Msaidizi wa Polisi SUZAN KAGANDA, amemtaja marehemu kuwa AMINA YUSUPH
aliyekuwa na umri wa miaka hamsini na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea
na upelelezi wa mauaji hayo.
via>>ITV
Social Plugin