MWANAMKE AUAWA KWA KUCHINJWA KAMA KUKU HUKO URAMBO TABORA

 

Watu wasiojulikana wamemuua kwa kumchinja mkazi wa kitongoji cha Kanoge kata ya Usisya wilayani Urambo mkoani Tabora.

Mwenyekiti wa serikali ya kujiji cha Mabunduru pamoja na ndugu marehemu wameelezea kusikitishwa kwao na kitendo hicho , kwani baada ya kumuua katika nyumba yake,watu hao hawakuchukua  chochote.
Diwani wa kata ya Usisya Mheshimiwa JAFARI KANKILA amesema tukio hilo ni la pili la wanawake kuuawa kwa kuchinjwa na ameahidi kutoa zawadi ya shilingi laki mbili kwa atakayetoa taarifa za kukamatwa kwa wahusika wa mauaji hayo.
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Tabora Kamishina Msaidizi wa Polisi SUZAN KAGANDA, amemtaja marehemu kuwa AMINA YUSUPH aliyekuwa na umri wa miaka hamsini na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi wa mauaji hayo.
via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم