NDEGE INAYORUKA KWA NGUVU YA JUA YAFANYIWA JARIBIO

1689 
Jaribio la kwanza la ndege inayotumia umeme jua limefanyika leo baada ya ndege hiyo kufanikiwa kuanza kuruka asubuhi ya leo.


Ndege hiyo iliruka majira ya saa 12 saa za Afrika Mashiriki ikianzia Abu Dhabi.

Marubani wawili wanaorusha ndege hiyo Bertrand Piccard na Andre Borschberg watapita katika hatua kumi na mbili za safari yao.

Duniani kote wataalamu wanaangalia namna ya kubuni teknolojia itakayosaidia kukabiliana na tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa, mpshi wa viwanda, magari vinatajwa kama vyanzo vya tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa.

Jaribio linafanywa sasa hivi likifanikiwa basi huenda historia ikaingia kwenye ukurasa mwingine, ndege inayotumia umeme wa nguvu ya jua imeanza safari ambapo tayari imeruka kutoka Abu Dhabi.
2011_04_06_Solarfirstflight2011_jrevillard_-30 
Ndege hiyo ina kiti kimoja ina mabawa yenye ukubwa kama wa ndege ya kawaida na uzito sawa na gari, mabawa yake yana solar panels ambazo zinasaidia kunasa nishati ya mwanga wa jua.
sunseeker_duo1-537x300 
Ndege hiyo ina betri zinazohifadhi nguvu ya umeme wa jua kutoka kwenye jua na hivyo itaweza kusafiri hata usiku, Andre Borschberg ndio rubani anayerusha ndege hiyo katika safari ya miezi mitano kuizunguka dunia, ambapo inakadiriwa umbali atakaosafiri ni zaidi ya Kilometre 35,000.

Ndege hiyo inasafiri na ujumbe wa kuhimiza uwekezaji kwenye Teknolojia salama ambayo ni rafiki kwa mazingira na ikifanikiwa kumaliza safari yake itaingia kwenye rekodi za kuwa ndege ya kwanza inayotumia nishati ya jua kusafiri duniani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post