Si jambo rahisi kwa mtu yoyote kufanya
maamuzi magumu kama haya ambayo wapenzi hawa waliamua kufanya ili tu
kutimiza ahadi yao ya kufunga ndoa.
Hayakuwa maamuzi mepesi kwa Jack Beniston kufanya dhidi ya mpenzi wake Michelle wanaoishi
Uingereza baada ya kupewa taarifa na madaktari kuwa msichana huyo
amebakiza masaa 48 tu kabla hajaaga dunia kutokana na kusumbuliwa na
maradhi muda mrefu.
Ndani ya masaa sita baada ya Jack kupewa
taarifa hiyo aliamua kuandaa harusi na kuifunga ndani ya chumba cha
hospitali ili kutimiza ahadi yake ya kufunga ndoa na binti huyo ambaye
alizaa naye mtoto mmoja aitwaye Martha.
Jack aliwaita marafiki pamoja na ndugu
zake ambao waliandaa sherehe ndogo ikiwa kumtafutia bibi harusi gauni
pamoja na pete ili aweze kutimiza ahadi hiyo.
Jack
alipata sapoti kutoka kwa ndugu zake,marafiki na hata manesi waliokuwa
wakimuuguza mpenzi wake ambapo walimwandalia sehemu nzuri akiwa
hospitali hapo na hatimaye akafunga ndoa na Jack.
Madaktari walisema Mishelle alikuwa
akisumbuliwa na kansa ya kizazi ambayo ilimtesa kwa muda mrefu na mwezi
Agust mwaka jana kuhamishiwa katika hospitali ya Peterborough City Hospital ambapo walidai ugonjwa huo tayari umemshambulia kwa kiasi kikubwa na hakuna uwezekano wa kupona
Baada ya kupewa taarifa ya kutoweza
kuona na mkewe Jack aliamua kufunga ndoa na Mishelle mwezi September na
baada ya kufunga harusi yake alifariki baada ya mwezi mmoja.
Social Plugin