Wekundu
wa Msimbazi Simba SC leo March 22, 2015,jioni , imezinduka kutoka
kwenye kipigo cha 2-0 cha Mgambo Shooting wiki iliyopita, baada ya
kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu 2014/2015 kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Simba
SC ilipata bao lake la kwanza dakika ya 60, mfungaji Ibrahim Hajibu
kwa mkwaju wa penalti, baada ya beki wa Ruvu, Said Madega kumfanyia
madhambi Awadh Juma.
Dakika moja baadaye ya 61, Awadh Juma aliifungia Simba SC bao la pili baada ya kujipasia mwenyewe na kupiga shuti.
Mshambuliaji Elias Maguri aliyetokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mganda, Emmanuel Okwi aliipatia Simba SC bao la tatu dakika ya 75, akimalizia pasi nzuri ya Said Ndemla.
Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 32 baada ya kucheza mechi 20, ikiwa nyuma ya Azam FC pointi 36 za mechi 18 na Yanga SC pointi 37 za mechi 18 pia.
Kwenye
mchezo mwingine wa Leo, Nao Mabingwa wtetezi ,Azam FC imeibuka na
ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani,
Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Shukrani kwake, mfungaji wa bao hilo Nahodha John Raphael Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 31 akimalizia pasi nzuri ya kiungo Mudathir Yahya.
Social Plugin