Khamis Mgeja |
Benson Mpesya
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja amesikitishwa na utendaji kazi wa mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya kwa kushindwa kusimamia kikamilifu kamati ya ugawaji chakula na vifaa hali iliyosababisha waathirika wa mvua ya mawe na upepo katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama,kugombea chakula na kulalamikia kuuzwa kwa magodoro na branketi zilizotolewa misaada na wahisani.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja amesikitishwa na utendaji kazi wa mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya kwa kushindwa kusimamia kikamilifu kamati ya ugawaji chakula na vifaa hali iliyosababisha waathirika wa mvua ya mawe na upepo katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama,kugombea chakula na kulalamikia kuuzwa kwa magodoro na branketi zilizotolewa misaada na wahisani.
Hayo yamebainishwa wakati kamati ya maafa ya mkoa ikipokea misaada
kutoka taasisi mbalimbali za fedha, mashirika na watu binafsi walioguswa
na kutoa misaada ya chakula, magodoro na nguo.
Mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja amesema kuwa endapo utendaji wa wakuu
wa wilaya kama alivyo mkuu wa wilaya ya Kahama usipobadilika Chama Cha Mapinduzi kitapata wakati mgumu katika
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa kuwa baadhi yao hawaendani na sera ya
chama.
Akijibu tuhuma hizo mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya
amesema kuwa yeye hausiki na upotevu wa vifaa vinavyodaiwa kuibiwa na
kuuzwa kwa watu wasiohusika na kusema kwamba rawama hizo zielekezwe
kwenye kamati ya maafa ya ugawaji.
Kufuatia hali hiyo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nasoro Rufunga
amelazimika kuingilia kati mgogoro huo na kuwaita wote kwa pamoja katika
kikao cha zarula ambapo hakutaka kubainisha hatua zilizochukuliwa na
kusema kwamba serikali imepokea maagizo ya kiongozi wa chama cha
mapinduzi na kuyafanyia kazi kwa lengo la kuhakikisha waathirika
wanapata huduma inayositahili.
Mkuu huyo wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya,anayedaiwa kutumia nafasi yake uongozi vibaya mbali na kuingia kwenye mgogoro na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga hivi karibuni aliingia kwenye mgogoro na mwandishi wa Habari wilayani Kahama.
Hii hapa Habari kuhusu Mgogoro wa DC na Mwandishi wa Habari
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mkuu wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, BensonMpesya mwishoni mwa mwezi Februari,2015 alitishia kumuweka ndani kwa saa 24 mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe, Mohab Dominic kwa madai ya kupuuza amri yake.
Sakata hilo lilitokea baada ya mwandishi huyo kukutwa amesimama nje ya ofisi za mkuu wa wilayahiyo muda mfupi toka alipofukuzwa kutoka ndani ya kikao kilichoitishwa kwa ajili ya makabidhiano ya hundi iliyotolewa na mgodi wa dhahabu wa Buzwagi ikiwa ni ada ya ushuru wa huduma kwa halmashauri zilizopo katika wilaya hiyo.
Kwamujibu wa taarifa ya mwandishi huyo iliyosambazwa kwa baadhi ya waandishi wahabari mkoani Shinyanga, hatua ya mkuu huyo kuagiza awekwe ndani saa 24 inatokanana kuchukizwa na kitendo cha kumkuta amesimama nje wakati aliisha mfukuza atokendani ya kikao kilichokuwa kikifanyika ndani ya ofisi yake.
Akifafanua katika taarifa hiyo mwandishi huyo alisema yeye pamoja na waandishi wenzake wengine kutoka
vyombo vya, Kahama FM, Mwananchi Communication Ltd, Mtanzania,ITV na Clouds FM walialikwa na uongozi wa mgodi wa Buzwagi kwa ajili ya kuhudhuria sherehe fupi ya kukabidhi hundi kwa halmashauri za Msalala naUshetu.
Hata hivyo alisema kabla ya shughuli ya makabidhiano hayo kuanza wageni wote waliokuwemo ndani ya ofisi ya mkuu wa wilaya walitakiwa kujimbulisha ambapo zamu yake ilipowadia ndipo mkuu huyo alipotoa amri iliyomtaka atoke nje mara moja huku akihoji ni mtu gani aliyemwalika.
Alisema pamoja na kumfahamisha mkuu huyo kwamba amealikwa na uongozi wa mgodi wa Buzwagi kuhudhuria sherehe hiyo fupi, alimjibu kuwa hataki kumuona ofisini kwake na hataki kufanya kazi na ambapo alimtaka atoke nje ya ofisi haraka ambapo alitii amri hiyo pasipo ubishi.
Alisema baada ya kutoka nje aliamua kuwasubiri waandishi wenzake ili watakapotoka waongozane pamoja na kuendelea na shughuli zao nyingine za kawaida ambapo ghafla wageni wote waliokuwa ndani ya ofisi ya mkuu huyo
walitoka nje ya ofisi hiyo kwa ajili ya kupiga picha ya pamoja ya ukumbusho.
“Wakati wageni wote pamoja na waandishi wa habari wakitoka nje kwa ajili ya kupiga picha ya pamoja ndipo mkuu wa wilaya aliponiona nikiwa nimesimama pembeni,ghafla alifoka na kuhoji kwa nini nilikuwa bado nipo katika maeneo hayo yaofisi na kunitaka niondoke maeneo hayo mara moja,” alieleza Dominick.
Aliendelea kueleza kuwa wakati bado akitafakari kitendo cha mkuu huyo wa wilaya kumtaka asionekane hata kwenye maeneo ya ofisi hizo za umma ,ghafla alimsikia akitoa agizo kwa mkuu wa polisi wa wilaya akimuagiza amkamate na kumuweka ndani saa 24 kwa kile alichodai kudharau amri yake.
“Kwa kweli nilishangaa kusikia mkuu wangu wa wilaya akitoa amri hiyo, na kweli OCD alinifuata huku akiniita, nilimuuliza iwapo sitakiwi hata kuwepo nje ya maeneoya ofisi hizo? Niliamua kuondoka ili kuepusha nisikamatwe pasipo kosa lolote la msingi,” alieleza Dominick.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo
Benson Mpesya akijibu kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi (sms) kupitia simu yake ya kiganjani alikiri kumfukuza mwandishi huyo na kufafanua kuwa kikao kile kilikuwa ni kikao cha ndani na kilihusisha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ambacho waandishi hawaruhusiwi.
Hata hivyo alipohojiwa kitendo cha waandishi wengine kuendelea kuwemo ndani ya kikao hicho, alisema walikuwa na kibali cha mwenyekiti bila ya kufafanua zaidi ambao waliendelea kushiriki katika shughuli hiyo na kushuhudia makabidhiano ya hundi hiyo ya shilingi 843,196,808 ikiwa ni ushuru wa huduma kwa halmashauri za Ushetu, Mji na Msalala wilayani Kahama.