Angalia Picha!! KAMPUNI YA SIMU TANZANIA YATOA MSAADA WA CHAKULA KWA WAHANGA WA MVUA YA MAWE HUKO MWAKATA KAHAMA

Hapa ni katika Shule ya msingi Mwakata moja kati ya kambi 3 za wahanga wa mvua ya upepo na mawe iliyoua watu 46 katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambapo leo ni siku ya 10 tangu kutokea kwa tukio hilo lililoacha simanzi siyo tu katika eneo hilo bali taifa zima la Tanzania.Leo Kampuni ya simu Tanzania -TTCL imewatembelea wahanga wa mvua hiyo na kutoa msaada wa vyakula ikiwemo mchele kilo 740,unga kilo 600,maharage kilo 300 na mafuta ya kula lita 260 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3.Wafanyakazi wa  TTCL mkoa wa Shinyanga ukiongozwa na Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru wamekabidhi msaada huo leo Machi 14,2015 kwa niaba ya Mkurugenzi wa shirika la simu Tanzania TTCL Dr. Kamugisha Kazaura
-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Magari ya Kampuni ya simu Tanzania -TTCL yalikuwa yamebeba vyakula kama vile mchele kilo 740,unga kilo 600,maharage kilo 300 na mafuta ya kula lita 260 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3.


Wafanyakazi kutoka Kampuni ya simu Tanzania -TTCL mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru (aliyevaa miwani kulia) wakijiandaa kushusha vyakula walivyokuja navyo kwa ajili ya wahanga wa mvua hiyo  inayojulikana kwa jina la TONADO.


Katikati ni  dereva wa Kampuni ya simu Tanzania -TTCL mkoa wa Shinyanga akisisitiza jambo kabla ya kukabidhi vyakula kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya anayepokea misaada mbalimbali kutoka kwa watu wenye mapenzi mema kwa niaba ya serikali na wahanga wa mvua hiyo.Nyuma yake ni meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru


Hizi ni miongoni mwa ndoo 26 za mafuta ya kula zilizotolewa na Kampuni ya simu Tanzania -TTCL baada ya kuguswa na tukio la mvua ya upepo na mawe iliyoua watu 46,kuua mifugo,kuharibu makazi na mazao mbalimbali


Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa chakula ambapo alisema TTCL inawapa pole sana wahanga wa tukio hilo na kwamba TTCL imepokea kwa huzuni kubwa tukio hilo na kuwataka Watanzania kuwaombea waliopatwa na janga hilo wapate faraja na kuwaombea kwa mwenyezi mungu waliopoteza maisha awapumzishe mahali pema peponi.Wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akisikiliza kwa makini


Meneja Kampuni ya simu Tanzania -TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa chakula kwa wahanga wa mvua ya Mwakata Kahama


Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru(aliyevaa miwani) akikabidhi mafuta ya kula kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya(aliyevaa suti kushoto),wa pili kutoka kushoto ni meneja mtandao TTCL mkoa wa Shinyanga Japp Mgalla,akifutiwa na dereva Adam Mgombewa,wa nne ni afisa utawala TTCL mkoa wa Shinyanga Dunstan Kaihula


Wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akipokea mfuko wa kilo 5 za mchele ukiwa ni miongoni mwa mifuko 148 sawa na kilo 740 zilizotolewa na TTCL mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kusaidia wahanga wa mvua ya ajabu iliyonyesha usiku wa kuamkia Machi 4,2015 huku ikiwa imembatana na upepo na mawe yanayodaiwa kuwa na uzito wa kilo 20
Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akizungumza baada ya kupokea msaada kutoka TTCL ambapo alilishukuru shirika hilo kwa kuona umuhimu wa kuwafikia wahanga wa mvua hiyo na kuongeza kuwa TTCL wamekuwa na moyo wa huruma kwa wahanga hao huku akiahidi kuwa misaada inayotolewa na watu wenye mapenzi mema itatumika kwa wahanga wa tukio hilo na sio vinginevyo na atakuwa mkali kwa hilo


Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akishikana mkono na meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru baada ya kukabidhi msaada wa vyakula,wa kwanza kulia ni meneja wa TTCL  wilaya ya Kahama bi Dollah Bhwana akishuhudia tukio zima katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga


Meneja wa TTCL mkoa wa Shinyanga Peter Kuguru akishirikiana na wakazi wa Mwakata na kikundi cha Skauti kushusha mifuko ya unga na mchele kutoka kwenye gari lililokuwa limebeba chakula hicho


Zoezi la kushusha chakula kutoka kwenye moja ya magari yaliyokuwa yamebeba vyakula kutoka Kampuni ya simu Tanzania -TTCL likiendelea


Wafanyakazi wa Kampuni ya simu Tanzania -TTCL mkoa wa Shinyanga wakishiriki zoezi la kushusha vyakula nje ya kambi ya muda ya wahanga wa mvua katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama


Wafanyakazi kutoka TTCL mkoa wa Shinyanga,Dereva Mesenja Seleman Bundala na dereva Idd Makota wakiwa katika kambi ya muda ya wahanga wa mvua ya Mwakata baada ya zoezi la kukabidhi vyakula kumalizika


Meneja wa Kampuni ya simu Tanzania -TTCL wilaya ya Kahama bi Dollah Bhwana akiwa na wafanyakazi wenzake na mwandishi wa habari Ndalike Sonda wa Baroha FM ya Isaka Kahama (kushoto)


Meneja wa TTCL wilaya ya Kahama bi Dollah Bhwana akiwa na  na mwandishi wa habari Ndalike Sonda wa Baroha FM ya Isaka Kahama na gazeti la Nipashe


Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akibadilishana mawazo na wafanyakazi wa TTCL mkoa wa Shinyanga baada ya zoezi la kukabidhi chakula kumalizika.


Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya ambaye leo siku ya 10 tangu kutokea kwa tukio hilo anahangaika huku na kule kuhakikisha kuwa wahanga wa mvua hiyo hawapati shida akiwasimulia wafanyakazi wa TTCL jinsi mvua iliyonyesha Mwakata ilivyokuwa na madhara makubwa kwa binadamu,mifugo na hata mimea


Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akiagana na wafanyakazi wa TTCL baada ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa wahanga wa mvua-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
KAMA HUKUONA PICHA ZA MAAFA YA MVUA HUKO MWAKATA BASI BONYEZA MANENO HAYA UONE PICHA ZAIDI YA 30

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم