Mabingwa
wa zamani wa ligi kuu ya Tanzania bara Dar es Salaam Young Africans,
ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Kimataifa
kunano kombe la Shirikisho barani Afrika, leo wamefanikiwa kutoa dozi
nzito kwa wapinzani wao Platinum Stars ya Zimbabwe kwa jumla ya mabao
5-1.
Katika
mchezo huo ambao umechezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam,
Yanga ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kunako kipindi cha kwanza
kupitia kwa Salum Telela, dakika ya 28 pamoja na Haruna Niyonzima,
dakika ya 44, lakini haikuchukua muda mrefu, Wazimbabwe hao
wakasawazisha kufatia adhabu ndogo, ambapo walipiga faulo na mpira
kuzama kimiani moja kwa moja katika dakika 45.
Licha
ya kukosa mabao mengi katika kipindi cha kwanza, ambapo zaidi ya nafasi
tatu za wazi washambuliaji wa Yanga walishindwa kuzitendea haki, Nyota
wa Burundi, Amisi Tambwe ikiwa ni dakika ya 46 yaani dakika moja tu
baada ya kipindi cha kwanza kuanza akafanikiwa kucheka na nyavu
akiandika bao la tatu (3) na kuamusha morali kwa wachezaji wa Yanga.
Yanga
wakizidi kushambulia kwa kasi lango la Platinum FC, ziliwachukua Dakika
tano (5) tu kwa mara ya nne, Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania
pamoja na klabu hiyo, Mrisho Ngassa ‘Uncle’ akaiandikia Yanga bao la 4
nakuzidi kuzamisha boti la Wazimbabwe hao.
ANGALIA PICHA NYINGI ZAIDI HAPA
ANGALIA PICHA NYINGI ZAIDI HAPA