Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

POLISI WAMSHUSHIA KIPIGO CHA MAANA KATIBU WA CCM HUKO SIMIYU

 
Polisi katika wilaya ya Meatu mkoani Simiyu imempatia kichapo cha nguvu jana usiku mjini Mwanhuzi,Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Simiyu,Jeremiah Shigala au Makondeko baada ya kuwazuia kufanya kazi yao walipokuwa wakimkamata mtu anayedaiwa mwizi wa Trekta.

Inaelezwa kuwa katibu huyo wa CCM  akiwa katika hotel ya Sengerema alifika eneo la tukio na kuzozana na askari hao na kisha kumpiga kichwa askari mmoja wakikosi cha usalama barabarani hapo ndipo walipompa kichapo hadi kumchania shati na kumtupa mahabusu.Chanzo cha habari jeshi la polisi Meatu.
Na Samwel Mwanga-Meatu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com