|
Rais Kikwete akisalimiana na kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa
Shinyanga baada ya kuwasili mjini Kahama katika uwanja wa ndege wa
Buzwagi kwa ajili ya ziara yake kuwatembelea wahanga wa mvua ilionyesha
Mwakata Kahama na kuua watu wengi.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete
leo amewatembelea na kuwafariji wahanga wa mvua ya mawe iliyoambatana upepo
iliyoua watu zaidi ya 40 katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama mkoani
Shinyanga hivi karibuni-picha zote na Marco Maduhu- Malunde1 blog Kahama |
|
Rais Kikwete akizungumza na baadhi wa wahanga wa mvua.
Akiwa Mwakata Rais Kikwete amesema serikali inatafuta
pesa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 403 kwa ajili ya waathirika wa mvua hiyo na
kuahidi kuwapatia chakula wahanga wa mvua hiyo.
|
|
Rais Kikwete akiwapa mkono wa pole baadhi ya wahanga hao.
Rais Kikwete amesema nyumba hizo zitajengwa na JKT ndani
ya siku 90 ambapo wanajeshi watalipwa na serikali-picha na Marco Maduhu- Malunde1 blog Kahama
|
Rais Kikwete pia alihutubia wakazi wa Mwakata
Picha Zote na Marco Maduhu- Malunde1 blog Kahama
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553