Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko
mkubwa na huzuni nyingi taarifa za kifo cha ghafla cha Mheshimiwa
Kepteni John Damian Komba, Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM na msanii hodari sana wa kizazi chake.
Katika
salamu zake za rambirambi kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Anne Semamba
Makinda na Katibu Mkuu wa CCM, Mheshimiwa Abdulrahman Kinana, Mheshimiwa
Kikwete amesema:
“Nimepokea kwa mshtuko mkubwa na huzuni nyingi taarifa za kifo cha ghafla cha Mheshimiwa Kepteni John Komba, ambacho nimejulishwa kuwa kimetokea mchana wa leo, Jumamosi, Februari 28, 2015, kwenye Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam.”

“Kwa
hakika, sina maneno ya kutosha kuelezea kwa fasaha hasara ambayo taifa
letu na chama chetu kimepata kutokana na kifo cha Kepteni Komba. Taifa
letu limepoteza hazina kubwa na mtu muhimu.
"Nimejua Kepteni Komba kwa muda mrefu sana, nimefanya naye kazi. Alikuwa msanii ambaye kiwango chake cha usanii kilikuwa hakipimiki, alikuwa na sifa kubwa za uongozi, alikuwa mpenzi, mzalendo na mtu mwaminifu sana kwa taifa lake na katika jambo lolote aliloliamini.,”amesema Rais Kikwete katika salamu hizo na kuongeza:

“Akiwa
mwalimu, lakini hasa akiwa Mlinzi wa Taifa katika Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ), Kepteni Komba alithibitisha sifa zake kama mlinzi wa
taifa kwa kipaji chake cha kutunga na kuimba nyingi za kuhamamisha
wanajeshi wetu katika ulinzi wa nchi yao.
"Alikuwa na uwezo mkubwa wa kisanii kutunga nyimbo za aina zote – ziwe za maombolezo, ziwe za kutoa hamasa, ziwe za makaribisho, ziwe za kampeni za kisiasa na kijamii ama ziwe za kampeni maalum.
"Alikuwa na uwezo mkubwa wa kisanii kutunga nyimbo za aina zote – ziwe za maombolezo, ziwe za kutoa hamasa, ziwe za makaribisho, ziwe za kampeni za kisiasa na kijamii ama ziwe za kampeni maalum.
“Mheshimiwa
Komba alikuwa Mbunge hodari sana na wananchi wa Nyasa wamepoteza
mtetezi wa uhakika. Mheshimiwa Komba alikuwa mcheshi, aliyependa sana
utani na alikuwa na uongozi mkubwa wa kutambua na kulea vipaji vya sanaa
na wasanii kama alivyothibitisha katika kuanzisha na kulea Kikundi cha
Tanzania One Theatre (TOT) na kabla ya hapo .
“Kupitia
kwenu Waheshimiwa, naomba mnifikishie salamu zangu za dhati kabisa kwa
Wabunge wote ambao wameondokewa na mwenzao na wananchi wa Jimbo la
Nyasa na Mkoa wote wa Ruvuma ambao wamepoteza mwakilishi na kiongozi
wao.
"Ndani ya Chama chetu, naomba salamu zangu ziwafikie wanachama wetu wote kwa kupoteza mwanachama mwenzao, ziwafikie viongozi na hasa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ambayo imepoteza mwakilishi mwenzao na wasanii wote wa Tanzania One Theatre (TOT) ambao Kiongozi wao ameondoka duniani,” amesema Rais na kumalizia:

"Naungana
na wanafamilia kuomboleza kifo cha rafiki yetu, ndugu yetu na kiongozi
mwenzetu. Napenda wanafamilia wajue kuwa natambua uchungu wao katika
kipindi hiki na tahayari yao ya kuondokewa na mhimili wa familia.
"Niko nao katika maombolezo na katika kumwomba Mwenyeji Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Kepteni John Damian Komba. Amen.”
"Niko nao katika maombolezo na katika kumwomba Mwenyeji Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Kepteni John Damian Komba. Amen.”
Social Plugin