Mwananchi akiwa amebeba moja ya barafu la mvua,yaliyokuwa yanadondoshwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo katika Kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga. Waliofika eneo la tukio Mawe hayo ya mvua yanadaiwa kuwa na ukubwa wa ndoo ya lita 10,na yalikuwa yamezagaa katika kijiji hicho baada ya mvua kukatika.Pichani ni barafu ikiwa imeanza kuyeyuka |
Watu 38 wamefariki dunia
na wengine 82 wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na nyumba kutokana na
mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo kunyesha usiku wa kuamkia leo
katika kijiji cha Mwakata Kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani
Shinyanga.
Mbuzi wakiwa wamekufa Mbuzi awakiwa wamekufa Vyakula vikiwa kwenye nyumba iliyoharibika |
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya
wilaya ya Kahama, ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo Benson Mpesya(mwenye suti) amesema
kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya itakaa kabla ya kamati ya mkoa ili
kupata taarifa zitakazoisaidia serikali kuanza kutoa misaada.
eneo la tukio
Viongozi wakiwa eneo la tukio
eneo la tukio
Viongozi wakiwa eneo la tukio
Nyumba ikiwa imeharibika vibaya,ambapo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga aliyefika eneo la tukio
Barafu maarufu MAWE ikiwa katika kijiji hicho baada ya mvua kukatika
Hali halisi katika eneo la tukio
Blog hii imefika katika eneo la tukio na kushuhudia nyumba za kaya mbalimbali katika kijiji hicho zikiwa zimebomoka na nyingine kuezuliwa mapaa huku hali ya mazao na miti ikiharibiwa vibaya na mvua hiyo ambayo pia imeuwa mifugo.
Moja ya nyumba zilizoharibika
Kijijini Mwakata
majaruba yakiwa yamefurika maji
madhara ya mvua hiyo
Madhara ya mvua
Mazao shambani
Miti imevunjika
Eneo la Mwakata
Jinsi Mimea ilivyoharibika
Hali halisi eneo la tukio
Akiwa eneo la tukio, Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha(pichani) amesema waliokufa wengi ni watoto ambao walisombwa na maji baada ya maji kujaa ndani ya nyumba zao na kwamba majeruhi wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama.
Wananchi wakihangaika
Kamanda Kamugisha amesema watu 35 wamekufa eneo la tukio na wengine wamekufa walipofikishwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama na kwamba idadi hiyo inaweza kuongezeka kutokana na majeruhi wengine kuwa na hali mbaya.

Mpesya amesema majina ya waliokufa kwa sasa bado hayajatambulika na kwamba kamati
ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Shinyanga inakaa jioni hii ili
kutathimini maafa hayo pamoja na kujua ni msaada gani unahitajika kwa
wahanga hao.
Akiwa eneo la tukio
Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya ametoa agizo kwa uongozi Redcross na jeshi la Scauti kuhakikisha
wanasaidia katika familia zilizokutwa na maafa hayo wakati serikali
ikisubiri kukamilika kwa zoezi la sense ya wahanga hao aliloagiza
kufanywa na viongozi wa eneo hilo.
Mwananchi akiwa haamini kilichotokea