|
Katika kuadhimisha wiki ya maji duniani leo Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wamefanya ziara katika chanzo cha mradi mkubwa wa maji ya ziwa Victoria cha Ihelele wilayani Misungwi mkoani Mwanza.Ziara hiyo imeandaliwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika mji wa Kahama na Shinyanga( Kahama Shinyanga Water Supply and Sanitation Authority( KASHWASA) lengo likiwa ni kuwajengea uelewa mkubwa waandishi wa habari kuhusu mradi huo.Wandishi hao wa habari walijionea chanzo cha maji katika ziwa Victoria,mitambo mbalimbali inayotumika kuzalisha maji hayo kisha kuyauza kwa mamlaka za maji katika miji ya Shinyanga na Kahama.-Picha zote na Kadama Malunde,Marco Maduhu na Stephen Wang'anyi-Shinyanga
|
|
Ziara ilianza kwa kikao katika ofisi za KASHWASA zilizopo katika kituo cha Kutibu maji yanayotoka katika ziwa Victoria,zilizopo kilomita chache tu kutoka ziwani,kikao hicho na ziara hiyo iliongozwa na
Mkurugenzi
mtendaji wa KASHWASA Injinia Clement Kivegalo akiwa ameambatana wataalam mbalimbali |
Mkurugenzi
mtendaji wa KASHWASA Injinia Clement Kivegalo akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema lengo la kuanzishwa kwa mamlaka hiyo mwaka 2009 ilikuwa ni kutatua changamoto ya maji katika mji wa Shinyanga na Kahama lakini hivi sasa miji mingi inahitaji maji hayo kama vile (MwanzaNgudu,Shinyanga na Tabora)baadaye Isaka,Kishapu,Kagongwa,Igunga na Tabora.Alisema wao ni wazalishaji wa maji wala siyo wasambazaji kwani kazi ya kusambaza maji kwa mteja mmoja mmoja inafanywa na mamlaka za maji katika miji husika kama vile KUWASA NA SHUWASA ambao ndiyo wateja wakubwa wa maji pamoja na kamati za maji za vijiji
|
HAPA NI KATIKA CHANZO CHA MAJI KATIKA ZIWA VICTORIA- Kulia ni
Mkurugenzi
mtendaji wa KASHWASA Injinia Clement Kivegalo akitoa maelezo kwa waandishi wa habari ambapo sasa wanazalisha lita milioni 80 kwa siku ingawa maji yanayotumika ni lita milioni 20 tu kwa siku kutokana na kukosekana kwa watumiaji wa waji,hali ambayo inawafanya wasizalishe maji mengi zaidi kutokana na kukosa wateja wa kutosha hivyo kulazimika kuzima mitambo kwani matanki yote yamejaa maji |
|
Tahadhari katika chanzo cha maji ya mradi wa maji ya Ziwa Victoria cha Ihelel,ukizubaa unaliwa na mamba |
|
Mkurugenzi
mtendaji wa KASHWASA Injinia Clement Kivegalo akizungumza katika chanzo hicho ambapo alisema maji ghafi kutoka ziwani husafirishwa kupitia mitambo mbali mbali na kuwekwa katika mazingira salama ya matumizi ya binadamu na hata mifugo. |
|
Waandishi wa habari wakiwa chanzo cha mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria |
|
Mkurugenzi
mtendaji wa KASHWASA Injinia Clement Kivegalo akiendelea kutoa maelezo muhimu kuhusu mradi huo |
|
Waandishi wa habari Kadama Malunde na Marco Maduhu ambao wanaomiliki mtandao huu wa Malunde1 blog wakapata fursa ya kupiga picha ya kumbukumbu katika Chanzo hicho cha Ihelele Mwanza |
|
Mfereji unaotoa maji ziwani kuelekea kwenye mitambo ya KASHWASA |
|
Hili ni jengo ambalo liko karibu na Ziwa ambako ndiko maji yanayotoka Ziwani yanaanza kuingia katika mitambo ya Kuzalisha maji |
|
Mkurugenzi
mtendaji wa KASHWASA Injinia Clement Kivegalo akitoa maelezo kwa waandishi wa habari katika chumba chenye mitambo mbalimbali kwenye jumba lililoko karibu kabisa na ziwa Victoria |
|
Baadhi ya mitambo katika jengo karibu na Ziwa Victoria,hii inatumika kusukuma maji hadi katika kituo cha Kutibu Maji cha Ihelele kilomita chache kutoka Ziwani |
|
|
BAADA YA KUTOKA ZIWANI HAPA NI KATIKA KITUO CHA KUTIBU MAJI TAKRIBANI KILOMITA 3.3 KUTOKA ZIWA VICTORIA
Jengo la utawala katika kituo cha kutibu maji
|
Mkurugenzi
mtendaji wa KASHWASA Injinia Clement Kivegalo akitoa maelezo jinsi maji Ghafi yanavyofika katika kituo hicho cha kutibu maji cha Ihelele |
|
Mkurugenzi
mtendaji wa KASHWASA Injinia Clement Kivegalo akiwa juu ya mitambo ya kutibu maji akitoa maelezo kwa waandishi wa habari
|
Picha ya kumbukumbu eneo la kituo cha kutibu maji
|
Mwandishi wa habari Shangwe Than akiwa juu ya mitambo ya kutibu maji cha Ihelele |
|
Mkurugenzi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde akiwa juu ya mitambo ya KASHWASA |
|
Ndani ya moja ya majengo yenye mitambo mbalimbali katika kituo cha kutibu maji cha Ihelele |
|
Mkurugenzi
mtendaji wa KASHWASA Injinia Clement Kivegalo akitoa maelezo juu ya namna mitambo hiyo inavyofanya kazi |
|
Mkurugenzi
mtendaji wa KASHWASA Injinia Clement Kivegalo ,nyuma yake ni tanki kubwa la maji ambayo yako tayari kwa ajili ya kupelekwa kwenye mlima wa Mabale ambako kuna tanki kubwa kwa ajili ya kusafirisha maji kwenda kwa watumiaji |
|
Kushoto ni afisa takwimu na huduma kwa wateja kutoka KASHWASA John Zengo Ngano,kulia kwake ni mkaguzi wa ndani kutoka KASHWASA Chrispino Koppa |
|
Hapa ni katika chumba cha kuchanganya dawa kwa ajili ya kutibu maji |
|
Kulia ni Gelard Benedictor akiwa na mkurugenzi wakitoa maelezo kuhusu mitambo ya umeme katika kituo hicho cha kutibu maji |
|
|
Fundi sanifu maabara kutoka KASHWASA Gelard Mgina akitoa maelezo wa waandishi wa habari kuhusu namna maji yanavyochujwa katika kituo hicho | |
|
|
Meneja Utawala na Rasilimali watu kutoka KASHWASA Denis Mulingwa akisisitiza jambo katika ziara hiyo |
|
Picha ya pamoja katika eneo la kutibu maji | | |
|
|
BAADA YA KUTOKA KWENYE KITUO CHA KUTIBU MAJI,SAFARI IKAELEKEA KWENYE MLIMA MABALE PICHANI-Katika mlima huo ndipo Kuna tanki kubwa sana lenye ujazo wa lita Milioni 35 za maji ambayo tayari yameshatibiwa kwa ajili ya kusambazwa katika maeneo mbalimbali kama vile Kahama na Shinyanga.Mlima huo una urefu wa mita 400 |
Mkurugenzi
mtendaji wa KASHWASA Injinia Clement Kivegalo akipanda juu ya tanki hilo ambapo maji yakifika hapo kuwa yanatoka menyewe bila kusukumwa na mtambo wowote,na presha yake ni kubwa sana
|
Maneno yanayomeka katika tanki hilo |
|
|
Waandishi wa habari wakiwa na
Mkurugenzi
mtendaji wa KASHWASA Injinia Clement Kivegalo juu ya tanki hilo japokuwa waandishi wengine hawakupanda kutokana na urefu uliopo katika tanki hilo lililopo juu ya mlima Mabale wenye urefu wa mita 400
|
Hapa ni juu ya tanki hilo kubwa sana
Waandishi wa habari waliopata ujasiri wa kupanda juu ya tanki hilo wakiwa juu ya tanki
|
Muonekano wa tanki la maji katika Mlima Mabale uliopo wilayani Misungwi mkoani Mwanza |
|
BAADA YA KUTOKA IHELELE-
Mkurugenzi
mtendaji wa KASHWASA Injinia Clement Kivegalo akiwa katika kijiji cha Lyabusalu jimbo la Solwa,ambako kunajengwa tanki la maji ya mradi wa maji ya ziwa Victoria |
|
HAPA NI KATIKA KATA YA MWAMALILI MANISPAA YA SHINYANGA- Waandishi wa habari wakiangalia mabomba yanatumika katika ujenzi wa mradi wa mji ya mtandao wa Ziwa Victoria ambayo yatapelewa wilayani Kishapu |
|
Afisa takwimu na huduma kwa wateja kutoka KASHWASA John Zengo Ngano akielezea kuhusu mradi wa maji hayo yatakayopelekwa wilayani Kishapu |
|
Afisa takwimu na huduma kwa wateja kutoka KASHWASA John Zengo Ngano akielezea zaidi kuhusu mradi ambapo tayari mitaro imeshachimbwa kwa ajili ya kulaza mitambo na wananchi wa Mwamalili watapata huduma ya maji hayo-Picha zote na Kadama Malunde,Marco Maduhu na Stephen Wang'anyi-Shinyanga |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553