Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JINSI CHADEMA WALIVYOFUNIKA SHINYANGA MJINI ,WAZINDUA OPARESHENI " SHAHADA MKONONI,DELETE CCM"








Hapa ni katika viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Nguzo Nane mjini Shinyanga ambako jioni ya leo mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amefanya mkutano mkubwa wa hadhara,ambapo maelfu ya wakazi wa Shinyanga wamehudhuria.Mambo mbalimbali yamezungumziwa katika mkutano huo likiwemo suala la katiba inayopendekezwa,daftari la wapiga kura,mauaji ya albino,rasilimali za nchi na mambo kadha wa kadha yanayohusu mstakabali wa taifa la Tanzania.Pamoja na hayo CHADEMA wamezindua Oparesheni Shahada Mkononi,Delete CCM-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga
Maelfu ya wakazi wa Shinyanga wakiwa katika eneo la mkutano wakimsubiri mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe
Mtoto Robert Donald akiwa amevaa nguo za Chadema eneo la mkutano


Awali mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Albinism mkoa wa Shinyanga Daniel Mabula akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka watanzania kuungana kwa pamoja kupiga vita vitendo vya mauajia ya albino huku akikisitiza kuwa albino haleti utajiri na kwamba wanaoua albino wanaleta balaa katika jamii.
Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika viwanja vya mahakama ya Mwanzo nguzo nane mjini Shinyanga leo jioni
Ulinzi ulikuwepo wa kutosha,askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga walikuwepo
Wafuasi wa CHADEMA wakisali kabla ya mkutano kuanza
Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Shinyanga Mjini Hassan Baruti akifungua mkutano
Mbunge wa viti maalum kutoka mkoani Mara Esther Matiko akizungumza na wakazi wa Shinyanga
Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Shinyanga Rachel Mashishanga akizungumza kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema Taifa Patrobas Katambi akiwasili katika viwanja vya mahakama ya mwanzo nguzo nane kwa ajili ya mkutano
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe akiwasili kwenye eneo la mkutano leo jioni
Mwenyekiti wa CHADEMA kanda Silvester Kasukumbayi akizungumza na wakazi wa Shinyanga
Mwenyekiti wa BAVICHA Patrobas Katambi akiwasalimia wakazi wa Shinyanga
Viongozi wa Chadema wakifuatilia kilichokuwa kinajiri uwanjani

Mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Ngokolo Diana Ezekiel akipanda kwenye baiskeli zilizogawiwa kwa viongozi mbalimbali wa kata wakati wa uzinduzi wa Oparesheni Shahada mkononi leo
Mheshimiwa Mbowe akimpatia Tisheti kiongozi wa kata wa Chadema leo
Mheshimiwa Mbowe akiendesha baiskeli baada ya kuzindua kampeni ya Shahada mkononi na kukabidhi baiskeli kwa viongozi wa kata watakazozitumia katika kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura
Wakazi wa Shinyanga wakifuatilia mkutano huo
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea

Mheshimiwa Mbowe akiwahutubia wakazi wa Shinyanga leo
Mbowe akizungumza na wakazi wa Shinyanga
Wakazi wa Shinyanga wakimsikiliza Mbowe
 Mwandishi wa habari akiandika dondoo muhimu


 Mkutano unaendelea
Maofisa wa polisi wakiwa eneo la mkutano karibu na meza kuu




Mheshimiwa Mbowe akiondoka eneo la mkutano baada ya mkutano kuisha-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com