Baraza la wanawake Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wilaya ya Shinyanga mjini( BAWACHA) wakiandamana kuelekea kwenye kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi (Albino) cha Buhangija mjini Shinyanga wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani,ambapo baraza hilo waliamua kuandamana kupinga vitendo vya mauaji ya albino nchini
-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Mwenyekiti wa Bawacha wilaya ya Shinyanga mjini Zenna Gulaam akiongoza maandamano hayo leo asubuhi wakitokea kwenye ofisi za Chadema wilaya ya Shinyanga-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog |
Maandamano ya amani kuelekea Buhangija yakiendelea-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Wakisubiri taratibu za kisheria zifuatwe ili kuingia ndani ya kituo cha watoto albino kutokana na ulinzi mkali uliopo katika eneo hilo,hatimaye wakaruhusiwa kuingia,wakiwa wamebeba msaada wa chakula ,mchele kilo 100 na sabuni za kufulia-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Mjasiriamali aliyekuwa ameambatana na akina mama wa BAWACHA,akiwa amebeba vyakula kwa ajili ya watoto hao-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Akina mama wa BAWACHA wakikabidhi msaada wa chakula katika kituo cha Buhangija ambacho sasa kinakabiliwa na uhaba wa chakula na malazi kutokana na idadi ya watoto hao kuzidi kuongezeka kila kukicha wakihofia kuuawa hivyo kukimbilia kituoni hapo kwa ajili ya kunusuru maisha yao-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Mwenyekiti wa Bawacha wilaya ya Shinyanga mjini
Zenna Gulaam amesema wameona
vyema siku hiyo ya wanawake duniani kuiadhimisha katika kituo hicho cha watoto
albino, ikiwa wao kama wazazi wana uchungu sana kusikia watoto hao wakiendelea
kuuawa na kukatakatwa viungo vyao, hali iliyowafanya kuiomba serikali watu
wanaotekelza mauji hayo wanyongwe-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Mwalimu Loyce Daudi akimshukuru mwenyezi mungu kwa kuendelea kusaidia watoto hao wanaoishi katika mazingira magumu waliotelekezwa na wazazi wao mara baada ya kukabidhiwa katika kituo hicho na kutorudi tena hali inayowafanya watoto hao waishi kwa kutegemea wasamaria wema-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Watoto wakiwa katika kituo hicho leo-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Viongozi mbalimbali wa BAWACHA wakiwa kwenye kituo cha Buhangija-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Social Plugin