Spika wa Bunge la County ya Nakuru Kenya, Susan Kihika amekimbia kutoka Bungeni baada ya vurugu kuibuka huku Wabunge wakimshutumu kwa uongozi mbovu.
Shughuli za Bunge zilianza kama kawaida na baadaye hali ilibadilika ghafla, Spika huyo akaanza kushambuliwa kwa matusi huku Wabunge wakosigelea meza yake kutaka kumpiga.
Hali hiyo ilitokana na Spika huyo kusoma
barua moja kutoka Mahakamani ambayo iliibua mzozo na kufanya kundi moja
la Wabunge kuanza kumshambulia na kutaka kumpiga hali iliyomfanya
akimbie nje akiongozana na walinzi wa Bunge na kupanda kwenye gaei yake
haraka na kukimbizwa kutoka eneo la Bunge hilo huku Wabunge
wakilikimbiza gari hilo.
Mzozo huo unatokana na ishu ya vikundi viwili kuzozana ndani ya Bunge kutokana na amri ya Mahakama kumtangaza Samuel Waithiki kama kiongozi badala ya Maura Njenga.
Wabunge wengine walibaki ndani ya Bunge wakimtaka Spika huyo ajiuzulu.
Unaweza kuisikiliza taarifa hiyo niliyoirekodi katika kituo cha K24 kwa kubonyeza play hapa.