WAKATI wapenzi wa muziki nchini Uganda wakiwa bado wamegubikwa na
simanzi kwa kuondokewa na mwanamuziki wa miondoko ya dancehall, Emmanuel
Mayanja maarufu kwa jina la AK47, taarifa mpya zimeibuka kuwa kuna
uwezekano kuwa alipigwa kabla ya kifo chake.
Jose Chameleon (katikati) akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na mdogo wake.
AK47 amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa hospitali baada ya kuanguka akiwa bafuni.
Taarifa hizo zinadai kuwa atakuwa alipigwa katika baa aliyokuwemo iitwayo Dejavu, iliyopo eneo la Kabalagala kabla ya kupelekwa Hospitali ya Nsambya, Kampala ambapo mauti yalimkuta.
Baa hiyo inamilikiwa na Jeff Kiwanuka, aliyekuwa meneja wa wasanii wawili Radio na Weasel.
Pallaso (mwenye tisheti ya bluu) ambaye naye ni kaka wa marehemu akifarijiwa na mwanamuziki Bebe Cool.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kabalagala, Nusulah Kemigisha
ameeleza kuwa anahisi kuna mchezo mchafu umechezwa baada ya kukuta mwili
wa marehemu ukiwa na majeraha sehemu za kifua na kuamua kufunga baa
hiyo ili kuruhusu uchunguzi ambao bado unaendelea mpaka sasa.
Marehemu AK47 enzi za uhai wake.
Imeelezwa kuwa AK47, ambaye ni mdogo wa mwanamuziki nguli wa Uganda,
Jose Chameleon (Joseph Mayanja), alipigwa na kuamua kwenda bafuni kunawa
kabla ya kudaiwa kuteleza na kuanguka.
Social Plugin