Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TIGO WAMWAGA ZAWADI ZA KUTOSHA MJINI KAHAMA,ZIMO MODERM ZENYE KASI ZAIDI 3G




Timu ya polisi Kahama mkoani Shinyanga imejinyakulia zawadi ya mbuzi na moderm 5 kutoka kampuni ya simu Tanzania TIGO baada ya kuibuka kidedea katika bonanza la  uzinduzi wa huduma ya internet yenye kasi zaidi (3G) kwa kuifunga timu kutoka idara ya maji wilayani humo KUWASA goli 2 kwa 1.

Katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa halimashauri ya wilaya ya kahama [uwanja wa taifa] ,polisi walianza kupata bao kupitia kwa Said Ramadhani dakika ya 8 na goli la pili likifungwa na Mbwana Ramadhani dakika ya 21 huku goli la kufutia machozi kwa Shuwasa likifungwa dakika ya 22 kupitia kwa David Kanyenye.

Baada ya mchezo huo kuisha kapteni wa timu ya poilisi Kahama Bahati Joseph amesema wamefurahishwa na bonanza hilo kutoka Tigo na hivyo kuiomba kampuni hiyo iendelee kufanya hivyo kwani michezo ni furaha pia amepongeza huduma zinanzo tolewa na kampuni hiyo ya Tigo hasa huduma ya internet.

Naye meneja wa huduma kwa wateja kanda ya ziwa kutoka kampuni hiyo ya simu Beatrice Kinabo amewashukuru wateja wao waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo halikadhalika na makampuni yote yaliyo jitokeza kushiriki bonanza hilo na hivyo kuahidi wataendelea kufanya mengi zaidi ili kuwanufahisha wateja wao.

“Nawashukuru sana wateja wetu pamoja na makampuni yote yaliyo shiriki bonanza hili la uzinduzi wa internet yenye kasi zaid 3G pia nawaahidi tutaendelea kutoa ofa nyingi kwa wateja wetu na zaidi kwa sasa tupo kila mahali”alisema Beatrice.

Katika bonanza hilo liloshirikisha timU 8 mshindi wa pili ambaye ni Shuwasa wamejinyakulia zawadi ya mbuzi na moderm 3,mshindi wa tatu ambaye ni Accese bank wamejinyakulia zawadi ya mordem 10 ambapo timu zingine  shiriki ni CRDB BANK,RDN,TURN ROAD KAHAMA,TIGO,na VETERANS KAHAMA.

Na Philipo Chimi-Malunde1 blog Kahama

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com