Ikiwa wiki hii ni wiki ya maji,Mamlaka ya maji safi na usafi
wa mazingira mjini Shinyanga(SHUWASA) Leo imefanya semina elekezi kwa waandishi
wa habari zaidi ya 20 wa manispaa ya Shinyanga kuhusiana na shughuli za mamlaka
hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya maji kwa mwaka 2015.Semina hiyo
imetanguliwa na Ziara kwenye Bwawa la Ning’wa na kwenye eneo la Mitambo ya
kutibu maji ya Ning’wa katika eneo Chibe manispaa ya Shinyanga ikiongozwa na mkurugenzi Mtendaji wa Shuwasa Injinia
Sylivester Mahole-Picha zote na Kadama Malunde na Stephen Wang'anyi -Malunde1 blog
|
ZIARA YA KUELEKEA NING'WA ILIANZIA HAPA-Waandishi wa habari zaidi ya 20 kutoka manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye gari kuelekea kwenye Bwawa la Ning'wa leo |
|
Walipata muda wa kubadilishana mawazo ndani ya gari aina ya Costa |
|
Maandishi yanasomeka ukifika katika Bwawa hilo la Ning'wa lililojengwa mwaka 1972 kwa ajili ya kuhudumia wakazi wa Shinyanga waishio maeneo ya Old Shinyanga,Ngokolo na Shinyanga mjini,Lakini sasa maji hayo yakitumiwa na manispaa yote ya Shinyanga. | |
|
|
|
Baada ya kuwasili Bwawani-mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA Injinia
Sylivester Mahole akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari. |
|
|
Bwawa hilo limeandamwa na magugumaji kama inavyoonekana pichani |
Wa pili kutoka kulia ni mhasibu SHUWASA Jovintus Rugemarila
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA Injinia
Sylivester Mahole akizungumza na waandishi wa habari katika Bwawa hilo ambako ndiko kwenye chanzo.Alisema bwawa hilo hivi sasa linakabiliwa na changamoto ya Magugumaji na kutokana na mabadiliko ya tabia nchi maji katika bwawa hilo yamepungua ingawa linauwezo wa kuhudumia wakazi wa mji wa Shinyanga kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja.
|
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA Injinia
Sylivester Mahole alisema mji wa Shinyanga unatumia maji ya bwawa la Ning'wa na maji ya ziwa Victoria na kwamba pindi maji ya ziwa Victoria yanapokatika bwawa hilo limekuwa mkombozi kwa wakazi wa Shinyanga |
|
Mwandishi wa habari Stephen Wang'anyi akitafakari jambo katika bwawa hilo |
|
Kushoto ni mhandisi wa maji wa SHUWASA Injinia Bundala Igambwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo ambapo pamoja na mambo mengine alisema bwawa hilo ni mbadala wa maji kutoka Ziwa Victoria,kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA Injinia
Sylivester Mahole |
|
Mwandishi wa habari Kadama Malunde akiwa kwenye bwawa la Ning'wa leo |
BAADA YA KUTOKA KWENYE CHANZO CHA MAJI/BWAWANI,HAPA NI ENE LA MITAMBO YA KUTIBU MAJI YA BWAWA LA NING'WA UMBALI WA KILOMITA 5.7-Waandishi wa habari wakaplekwa eneo hilo kujionea namna maji yanatoka kwenye bwawa yanavyochujwa na kutibiwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu na hata mifugo.Kituo hicho cha kutibu maji kilianza kufanya kazi mwaka 1988
Kushoto ni mhandisi wa maji wa SHUWASA Injinia Bundala Igambwa akiwaeleza waandishi wa habari namna maji yanavyotibiwa
Mhandisi wa maji wa SHUWASA Injinia Bundala Igambwa akitoa ufafanuzi namna maji hayo yanavyotibiwa/kuchujwa kupitia chemba mbalimbali katika eneo hilo
|
Waandishi wa habari wakipita juu ya mitambo ya kutibu maji |
|
Waandishi wa habari wakiwa juu ya mitambo ya kutibu maji |
|
Mhandisi wa maji wa SHUWASA Injinia Bundala Igambwa akiendelea kutoa maelezo |
|
Mhandisi wa maji wa SHUWASA Injinia Bundala Igambwa akiendelea kutoa maelezo |
|
Sehemu ya kutibu maji yanayotoka Ning'wa kwa ukaribu zaidi |
|
Mhandisi wa maji wa SHUWASA Injinia Bundala Igambwa akiwa kwenye chumba cha kuzalisha upepo katika eneo la mitambo ya kutibu maji |
|
BAADA YA ZIARA SEMINA IKAENDELEA KWENYE UKUMBI WA VIJANA CENTER MJINI SHINYANGA-Aliyesimama ni mgeni rasmi bi Paulina Limbe ambaye ni mjumbe wa bodi ya Shuwasa akiwakilisha akina mama watumiaji wa maji na walipaji kodi akifungua semina elekezi kwa waandishi
wa habari zaidi ya 20 wa manispaa ya Shinyanga kuhusiana na shughuli za Mamlaka ya maji safi na usafi
wa mazingira mjini Shinyanga(SHUWASA) |
Mgeni rasmi bi Paulina Limbe akitoa hotuba yake katika semina hiyo ya siku moja kwa waandishi wa habari
Waandishi wa habari wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
|
Afisa uhusiano SHUWASA bi Nsianeli Gelard-Picha zote na Kadama Malunde na Stephen Wang'anyi -Malunde1 blog |
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin