Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Tunaomba Radhi kwa Picha Hizi!! MTOTO WA AJABU AZALIWA SHINYANGA,HANA MDOMO WALA PUA,MASIKIO YAKO SHINGONI



 Mwanamke mmoja mkazi wa manispaa ya Shinyanga amejifungua mtoto wa ajabu wa kike asiyekuwa na mdomo wala pua huku masikio yake yakiwa shingoni katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.



 Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga  Dkt Mfaume Salum amesema mtoto huyo alizaliwa jana saa moja asubuhi na alifariki muda mfupi baadaye kutokana na kasoro alizokuwa nazo.
Mwandishi wa Malunde1 blog Nunu Abdul amezungumza na mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt Mfaume Salum.

"Ni kweli mwanamke huyo alijifungua mtoto mwenye mapungufu katika viungo vyake hasa kichwani,hii huwa inatokea mara kwa mara kwa kila vizazi hai 33,kunaweza kukawa na mtoto mmoja mwenye tatizo kama hili,lakini hali hii inatokea kwa sababu ya vinasaba hasa katika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito wa kwanza",alieleza Dkt Mfaume.


"  Katika miezi hiyo mitatu mara nyingi ndiyo kuna utengenezwaji wa viungo mbalimbali vya mwili na hali hii pia husababishwa na utumiaji wa dawa zisizoruhusiwa wakati wa ujauzito",aliongeza.

Dkt Salum amewataka akina mama wanapokuwa wajawazito kuhudhuria hospitali mapema pale wanapojisikia kuwa wajawazito ili kupata maelekezo juu ya matumizi ya dawa mbalimbali.

Amesema hali hiyo kwa kitaalam inaitwa Congenital malformation.

Hata hivyo mganga huyo amekanusha uvumi ulionea mtaani kuwa kuzaliwa kwa mtoto wa ajabu kama huyo inatokana na utumiaji wa njia za uzazi wa mpango.

Na Nunu Abdul-Malunde1 blog Shinyanga 
BOFYA HAPA KUSOMA HABARI YA MWANAMKE KUJIFUNGUA NYOKA HUKO DAR 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com